Baada ya watu kibao kujitokeza kufanya audition ili kushiriki katika
tamthilia ambayo imejishindia tuzo , Vanessa Mdee ametajwa kama moja ya
washiriki ambao watahusika katika tamthilia hiyo ya Shuga sehemu ya
tano.
MTV Shugar ni tamthilia ambayo inaelezea mapenzi, muziki, mahusiano na
Drama ambavyo vyote hivi ni moja ya issue ambazo zinawazunguka watu
katika maisha yao ya kila siku, baada ya season nne kufanyika Kenya na
Nigeria, inakuja tena kwa mara nyingine South Afrika kama sehemu ya 5
huku ikiongozana na Vanessa Mdee, Thuso Mbedu, Mohau Mokoatle Cele, Jezriel Skei, Emmanuel Ifeanyi, Nick Mutuma na Adesua Etomi wakiwa na crew nzima ya MTV Shuga.