Kama tulivyowazoea mastaa wengi wa Afrika na hata wale wasanii wakubwa nchini marekani.
Yemi Alade na Davido
Hii tofauti kabisa kwa mshindi wa tuzo lukuki za kimataifa Yemi
Alade, kwani wiki hii wakati ana’cover jarida la fader Magazine
aliulizwa swali ni kwa nini hatumii Pesa kama Davido au kama mastaa
wenzake wakubwa wa Nigeria?Yemi Alade alianza kwa kusema “Kwa mtu ambae hujatoka kwenye familia ya kitajiri kama Davido ni ngumu sana kufikia malengo yako” Yemi Alade alianza kwa kusimulia historia yake ya maisha.
“Oooohhh natakiwa nitafute zaidi kwani kuna tofauti kubwa sana kati ya Yemi Alade na Davido, Utakuwa hujakosea ukimuita Davido ni Mtoto wa Kitajiri.” Yemi Alade aliendelea kusema.
“Kwa upande wangu ni Tofauti kabisa, Historia zetu za maisha zinatofautiana kabisa hivyo ni lazima tutofautiane kwenye matumizi. Yeye (Davido) lazima atafute Gari lenye thamani kubwa zaidi Duniani lakini mimi natafuta gari lolote lile ilimradi linifikishe safari.“ Aliendelea, na alizidi kwenda mbali zaidi kwa kusema.
Kabla ya Baba yangu kufariki siku moja aliniletea Bakuli ambalo lilikuwa na maharage ambayo yalikuwa yamechanganyika changanyika na kisha kuniambia unaona nini humu kwenye bakuli..? nikamjibu naona mchanganyiko wa maharage ambayo yamepondeka pondeka na mengine hayajapondeka kabisa. Basi akachukua lile bakuli akaanza kulitikisa baada ya muda akanionesha tena akaniambia unaona nini…?nikamjibu naona mchuzi mzito juu ya bakuli, Basi akaniambia ili ufanane na wao lazima utumie nguvu, Nikanoti hiyo kauli hadi leo hii.”
Yemi Alade alikuwa nchini Marekani wiki hii aki’cover stori kwenye Jarida la Fader Magazine baada ya kutangazwa kuwa ni Malkia wa Afrobeats kwa mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment