Friday, November 11, 2016

Nikki Mbishi awajia juu Roma na Tongwe Records, adai Roma kaiba mistari yake kwenye ngoma hii(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Rapa kutoka kundi la Tamaduni Muzik Nikki Mbishi leo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ametoa ya moyoni na kudai ya kwamba rapa mwenzake Roma mkatoliki kutoka Tongwe Records ametumia mashairi ya wimbo wake kwenye Cypher
ya Fiesta 2016.
Nikki Mbishi aliandika kwa kuanza kulaumu studio za Tongwe Records kwa kuchelewesha kutoa ngoma zake kwani ndiyo chanzo cha mashairi yake kuibiwa na Roma.
Nikki Mbishi
“Tongwe Records Bwana tunarekodi mangoma makali hawayatoi yapo tu ndani, matokeo yake Roma anachukua Verses za watu anachana yeye!“ aliandika Nikki Mbishi kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Aliongeza pia kwa kuandika
“Baada ya kuchana verse yangu kwa jina lake, akarusha na label, so pengine Biggie kamkaribisha Diddy na bad boy”
Hata hivyo Tongwe Records wamemshauri Nikki Mbishi kukaa pamoja na Roma badala ya kuendelea kuchafua Brand yao ya Tongwe Records, kwani wizi huo sio wa Tongwe Records.
Roma nae mpaka sasa hivi hajajibu chochote kuhusu tuhuma hizo za wizi wa mistari.

No comments:

Post a Comment