Tuesday, November 8, 2016

Alichokisema Alikiba baada ya kudai kudhulumiwa kwenye tuzo za MTV EMA(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Ni juzi ndiyo siku ambayo zilikuwa zikitolewa tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) ambapo bendera ya Tanzania ilikuwa ikipeperushwa na mkali Alikiba pande hizo.
Ni Best African Act ndio category ambayo mtu mzima kiba alikuwa akigombania pamoja na mastaa wengine wakubwa Africa akiwemo Wizkid wa Nigeria ambaye ndiye aliye tangazwa kama mshindi wa category hiyo.
Kitu ambacho kimezua utata ni baada ya kura kuonyesha dhahiri kuwa Alikiba ndiye mshindi halali wa tuzo hiyo na kama ilivyokuwa katika categories zingine kuwa mwenye kura nyingi ndiye anapewa tuzo lakini kwenye category hiyo ushindi alipewa Wizkid ikiwa kura aliongoza msanii Alikiba.
Imewagusa wengi wapenzi wa muziki mzuri na kuwaweka katika hali ya sintofahamu kutokana na kitendo hicho.
  Jana Alikiba alikuwepo katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, na moja kati ya maswali ambayo aliulizwa mkali huyo ni pamoja na hilo la kuhusu MTV EMA.

No comments:

Post a Comment