Monday, January 2, 2017

Nikki Mbishi afunguka kuhusu hali ya Nando, ‘alipaswa kuwa mfanya biashara mkubwa’ (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Wengi tunamfahamu Nando, nyota kutoka Tanzania aliyewahi kushiriki shindano la Big Brother Afrika-The Chase, hali yake imekuwa mbaya kutokana na madawa ya kulevya na imemfanya Rapper Nikki Mbishi kuongea mengi.

Baada ya picha kibao kusambaa mitandaoni zikimwonyesha Nando kwenye hali mbaya, Rapper Nikki Mbishi anahuzunishwa na matatizo ambayo rafiki zake wanakutana nayo kwa kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kuwafanya kupotea katika michongo yao ya kimaisha hadi kupelekea Nikki kujiuliza kwanini Mungu?, Kupitia kurasa yake Instagram, Nikki Mbishi amefunguka mengi kuhusu Nando kwamba anamtaka aachane na matumizi hayo, kwasababu alikuwa anaamini kwamba hatua ambayo Nando aliifikia ilipaswa awe mfanya biashara mkubwa.
‘nikkimbishi#NANDO stop whatchu doin bruh,get off whatchu on to!  I’d like to see u this effectively healthy.  Hatua uliyofikia ulipaswa kuwa mfanya biashara mkubwa due to the huge exposure you got for reppin’ yo country in #BBA.  Come back to the essence of time home boy.  Mkono wa Mungu na ukuguse na usisite kugeuka ukiguswa,sipendi picha zako zinazosambaa mitandaoni,jifunze kupitia kaka zako waliopotea kwenye hayo mambo.  #UNLUCKY_ME  Most of my friends are unfortunately dragged into drugs but why GOD?  Be Blessed and happy new year!’ Aliandika Nikki Mbishi.

Yemi Alade kuhusika kwenye tuzo za Grammy (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Wakati mashabiki wa muziki Afrika nzima wakiwa wanasuburia tuzo ya Grammy kutoka kwa Wizkid kupitia wimbo wa Drake wa “One Dance”, Yemi alade amepokea mwaliko wa kuhudhuria tuzo hizo.
Afrika inazidi kusonga mbele na kufanya vizuri kwenye sekta ya muziki kwa kuwakilishwa na wasanii kibao kutoka kila pande ya Afrika, Sasa msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade anayetamba na kibao chake cha “TumBum”, ameamua kushare na sisi mwaliko wake alioupata kwa ajili ya kuhudhuria tuzo za Grammy zinazotarajiwa kufanyika Mwakani February 12 siku ya jumapili.