Fid Q amesema zama za wasanii wa hip hop kufanya video rahisi umepitwa
na wakati na kwamba wasanii sasa wanatakiwa kuumiza vichwa zaidi.
Fid Q
Amedai kuwa mashabiki wa sasa wanataka kuona video ambayo inaweza kuwavutia machoni.“Ni muda mrefu sana wasanii wa hip hop wamekuwa wakifanya video simple tu, ndio hip hop is the realness of reality lakini tunaishi katika zama ambazo biashara imetoka kwenye showbiz inaenda mpaka kwenye eye-candish – ni kwamba watu wanataka waangalie kitu ambacho macho yao yatavutiwa, yapata ladha fulani,” alisema Fid
Hivi karibuni Fid Q ameonesha kulizingatia hili kwa kutoa video zenye viwango tofauti na zile alizokuwa akizitoa mwanzo.
No comments:
Post a Comment