Ushindi wa tuzo ya Alikiba kwenye tuzo za MTV EMA ambayo awali alipewa
Wizkid umefichua mambo mengi kiasi cha kuanza kuwapa wasiwasi wasanii wa
Tanzania.
Jux ameamua kufunguka ya moyoni kwa waandaji wa tuzo hizo, huku
akiwalaumu kwa kuacha watu wapige kura huku washindi wanawapendekeza
bila ya hata kuzingatia kura za mashabiki. Jux anaamini kama zoezi la
upigaji kura kwenye MTV EMA lisingekuwa wazi Alikiba asingeshinda tuzo
ambayo anastahili.
Jux pia amesema polls za upigaji kura kwenye tuzo za MAMA’s nzo
zingekuwa wazi basi tuzo hizo zingerudi nyumbani, amedai kuwa anaamini
Diamond alishinda lakini walimpa Wizkid.
No comments:
Post a Comment