Friday, November 25, 2016

Mwana Fa: Vita za kimuziki ni sehemu ya kukuza kazi ya Sanaa(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Vita ya Diamond na Ommy Dimpoz ni moja ya vita ambayo imefanya mashabiki wengi kuwa na maswali , ila kwa upande wa Mwana Fa yeye anajibu moja tu kwamba upinzani ni sehemu ya kukuza kazi ya sanaa.
Baada ya kuachia Dume Suruali ambayo inatarajiwa kufanya vizuri kwenye chart za Bongo mpaka nje ya nchi, Mwana Fa ameamua kufunguka juu ya vita ambayo imeibuka kati ya Ommy Dimpoz pamoja na Diamond.
Mwana Fa aliamua kufunguka na kusema kwamba mambo ya vita kati ya wasanii wetu hatujaanza kuyaona kwenye muziki wetu peke yake, ishu kama ya Siasa, Mpira hata vyombo vya radio vyote hivi vimekuwa vikikutana na vita ambazo wao kama wao zinakuwa zinawaongezea manufaa kiuchumi.
Upinzani na vita ni moja ya mambo ambayo kwa asilimia fulani yanaweza kukuza kazi ya sanaa, kwasababu hapo ndipo juhudi zinapatikana kwa wasanii wetu ilikuongeza waweze kukua kimuziki.

No comments:

Post a Comment