Baada ya kushika chati na album ya pamoja na rapa Fat Joe, Remy Ma
ambaye tayari kushatoka kama solo artist na ngoma zake mbali mbali.
Remy Ma
Kwenye mahojiano wiki hii rapa Remy Ma aliyesikika sana kupitia wimbo
wa “All The Way Up” na Fat Joe, amesema hapakuwa na kazi iliyo fanyika
kati yake na Nicki Minaj.Remy anasema “Nilipotoka jela Minaj alinipigia simu na tukapanga colabo ila alisema iwe siri na baadae yeye ndio akaivujisha hio siri, kama alitaka wimbo na Foxy Brown angefanya mapema hata bila mimi, watu wanajua tuna vipaji na wanataka kuona vikiwa pamoja ila kwenye maongezi yetu nili muambia kuwa watu wata tugombanisha na ndio kinachotokea sasa ila sina dhima ya kumdiss mtu bila sababu”
Wiki mbili zilizopita Nicki Minaj alisema kuna collabo kati yake na Remy Ma na imetayarishwa na Diplo.
Remy pia anasema ni muda wasanii wa kike waache majigambo yao ili tufanye kazi pamoja kama wakina Drake, Rick Ross, na French Montana wakifanya colabo inakuwa kubwa sana.
No comments:
Post a Comment