Friday, November 25, 2016

Ben Pol-: Mimi sihitaji KIKI ili muziki wangu upenye (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Ni kwenye Clouds E ya Clouds TV na Shadee Weriss ambapo Ben Pol alikuwa na interview kuzungumzia muziki mpya ambao ameshirikishwa na Darassa unaoitwa Muziki.
Ben Pol amefunguka kuwa kwa kipindi hiki ambacho ni ngoma kibao zimetoka kwa mkupuo itachukua takriban wiki 3 ili ngoma hizo kujichuja na muziki mzuri kuendelea kuishi muda mrefu zaidi ya hapo  na zingine ambazo zimetoka kwa kiki kuishia hewani.
“Sisi hatuhitaji kiki ili muziki wetu kupenya, siku zote muziki ambao unatoka kwa kiki sio muziki mzuri, inadhihirisha kuwa muziki huo haujitoshelezi ndio maana unatafutiwa kiki ili kuupa nguvu.” Alisema Ben Pol.
Tangu wiki hii imeanza ni zaidi ya ngoma 5 zimeshaachiwa ikiwa ni pamoja na Dume Suruali ya Mwana FA na Vanessa Mdee, Nitampigia ya Stamina na Mr Blue, Kokoro ya Rich Mavoko na Diamond, Muziki ya Darassa na Ben Pol pamoja na  Mwendo Tu wa Songa na Jay Moe.

No comments:

Post a Comment