Baada ya Hillary Clinton kushindwa katika
uchaguzi mkuu nchini Marekani dhidi ya Donald Trump, nyota wa muziki
nchini humo, Jay Z na mke wake, Beyonce, wamemtaka mke wa Barack Obama,
Michelle Obama, awanie kiti hicho 2020.
Jay Z na Beyonce
Wasanii hao walikuwa wanamsapoti Hillary katika uchaguzi huo na
walikuwa wanaungana baadhi ya sehemu kwa ajili kumnadi, lakini
hajafanikiwa kushinda, hivyo wawili hao wameamua kuangukiakwa mke wa Obama, Michelle, kuwa awanie nafasi hiyo mwaka 2020 wataungana pamoja kwenye kampeni.
Michelle na mume wake, Obama, ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanampigia debe Hillary, lakini hawakufanikiwa.
Novemba 7 mwaka huu, Jay Z aliachia wimbo
mpya ambapo ndani yake kuna mistari inasema kuwa anataka mtoto wake akue huku akiwa anaongozwa na rais mwanamke na hivyo walitamani kuona Hillary kupata nafasi hiyo.
“Nilitamani kuona mtoto wangu akiwa anakua chini ya rais mwanamke, Hillary hajapata nafasi hiyo, lakini ninaamini bado kuna nafasi nyingine
baada ya miaka minne ijayo, nimekuwa nikiongea na Michelle mara kwa mara na ninaamini atafanya hivyo,” alisema Jay Z.
No comments:
Post a Comment