Sunday, November 13, 2016

Hatimaye Series ya mauaji ya 2 Pac na BIG kutua kwenye TV(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Wakati mashabiki wanasubiri filamu ya maisha ya Tupac, All Eyez On Me itoke, USA Networks, imetangaza kuwa itaachia drama ya uhalifu wa
kweli kuhusu mauaji ya Pac na The Notorious B.I.G.
Vifo vya Shakur na Biggie vimewahi kuandikwa kwenye vitabu vingi na documentaries kadhaa.
2 PAC & B.I.G
Series hiyo itajulikana kwa jina la Unsolved, The Hollywood Reporter imeripoti kuwa series hiyo
itatoka ndani ya miezi 12 ijayo.
Series hiyo itajikita kwenye kazi ya mpelelezi wa LAPD Detective Greg Kading, aliyeongoza uchunguzi wa mauaji hayo.
Mpelelezi huyo alishawahi kuandika pia kitabu kiitwacho Murder Rap: The Untold Story of Biggie Smalls & Tupac Shakur. Murder Investigations, ambayo ilifanyiwa documentary yenye jina hilo pia.

No comments:

Post a Comment