Tuesday, November 29, 2016

album mpya ya Navy Kenzo “AIM” (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Ebhana AIM ndio album ya kwanza ya Afro pop ambayo inategemewa kutoka mwaka huu mwezi Disemba, na hii ikiwa katika kipindi ambacho wasanii wengi na record label hawaamini juu ya album kutokana na wasambazaji kuwa wachache.
Akiongea na Perfect255, muhudumu wa mauzo ya Album ya AIM, amefunguka na kusema kwamba kwa sasa wanapokea pre order ila pia wameweka katika vituo mbalimali ambavyo vitakuwa ni kuponi ambazo zinakodi, kwahiyo mtu akitoa order yake anapatiwa koponi yake.
“Kwa sasa tunachukua pre order, lakini tumeweka pia kwenye vituo mbalimbali ambazo sisi tumeweka kitu kinaitwa kuponi, kuponi hizo zinakuwa na kodi ambazo mtu akitoa order yake anapewa hiyo kuponi, tumefanya syteam ambayo inaitwa pre order ili iweze kumfikia kila mtu, nikimaanisha kwamba Pre order unaweza kulipia hata nusu, hata robo kwamba ninauwakika nitaichukua hii album, yaani unaweza kulipa kwa vibubu mpaka pale utakapomaliza order yako…….Usambazi tutafanya wenyewe kama wenyewe, Album ikishatoka bei nayo itaongezeka na ndio maana tumeweka pre order, kwahiyo ile namba ambayo tumeweka pale mtu ndio atatumia kununua kutuma pesa yake, picha yake kama akitaka tumposti na akaunti yake ya Instagram….mpaka sasa tumepata sapoti kubwa ambayo kila msanii amekuwa akinunua kuonyesha love..na wasanii wengine ambao watakuwepo kwenye album yetu pia tutawatangaza kupitia XXL.”
Album ya AIM unaweza kupreorder kwa gharama ya 10,000tzs na unaweza kutoa oda yako kwa kutumia namba ya simu ya +255656762983 ili kuenjoy album yako ya AIM.

No comments:

Post a Comment