Muongozaji huyo na mtayarishaji wa video nchini Hanscana, amesema sababu inayo pelekea video nyingi za bongo kurudiwa na kufanana ni kutokana na maamuzi na mapendekezo ya msanii mwenyewe anacho pendelea.
Hanscana
Akipiga story ndani ya eNewz amesema “Ukiona kuna kitu
kimerudiwa katika video ujue kuna makubaliano kati ya muongozaji na
msanii kwa kuwa mara nyingi msanii anapo andika wimbo wake anakuwa na
wazo la aina ya video ambayo anaitaka hivyo wasanii ni kama wateja wetu
na tunafanya anachokitaka mteja wetu”.Pia Hanscana amesema kwamba yeye na Khalfani ni marafiki japo hawajawahi kufungua kampuni moja ila wakati wanatafuta maisha waliwahi kuishi nyumba moja kwa sasa kinacho watenganisha ni kutokana na kila mmoja kuzidi kutafuta maisha yake japo bado ni marafiki.
No comments:
Post a Comment