Friday, November 4, 2016

Mwana FA huenda akaachia ngoma mbili kwa mpigo, ikiwemo remix ya Asanteni kwa kuja (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Kwa muda mrefu, Mwana FA amekuwa akizungumzia kuja na remix ya wimbo wake, Asanteni kwa Kuja.
Hivi karibuni alidai kuwa ni mtu mmoja tu aliyekuwa hajamalizia kuingiza verse yake lakini wote aliowashirikisha wamekamilisha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, rapper huyo amewauliza mashabiki wake kama wanataka aachie remix hiyo au atoe ngoma nyingine.
Mashabiki wamekuwa na mtazamo tofauti lakini kuna uwezekano akaja kutoa ngoma zote mbili. Ni kwasababu mkali huyo amemaliza kushoot video ya wimbo wake mpya nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment