Monday, October 31, 2016

Majibu ya Kala Jeremiah kuhusu remix ya “Wanandoto” na mashabiki.(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Takriban miezi miwili sasa imepita tangu msanii wa Hiphop Kala Jeremiah alipotoa ahadi ya kufanya remix ya wimbo wake wa “Wanandoto” na mashabiki zake wenye vipaji na kutoa tamko la kwamba mashabiki hao wawe wanajirekodi video fupi huku wakiimbia beat ya Wanandoto kwa kutumia mistari yao binafsi na kupost katika kurasa zao za instagram na kuweka hash tag ya Wanandoto (#Wanandoto).
 “Project ya wanandoto remix inaenda vizuri na washiriki wote 8 wamekwisha ingiza sauti, kutoka mikoa mbali mbali na mmoja kutoka Kenya. Imebaki tu sehemu yangu mimi kwasababu nina kama miezi miwili sipo Dar, niko mikoani kuna kazi fulani naifanya na hivyo mimi ndio nimekuwa kama kikwazo katika ucheleweshwaji wa hii project. Lakini all & all mwishoni mwa mwezi wa 11 narudi Dar es Salaam na kitu cha kwanza ni kwenda studio na kukamilisha hicho kitu na baada ya hapo process zingine zitafuata.”Asema Kala Jeremiah

No comments:

Post a Comment