Rapa Lord Eyes ambaye ni mmoja wa wasanii wa kundi la Weusi
amefunguka na kusema msanii Ray C bado ana chumba chake kwenye muziki na
kusema yeye bado anamuombea kwani kwa matatizo aliyonayo kwani yale ni
kama maradhi hivyo hayaponi kwa siku moja.
Lord Eyes ambaye kwa sasa amepumzishwa
kwenye kundi hilo, alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ kinachorushwa
na EATV na kusema kuwa mpaka sasa yeye hawasiliani wala kuongea na Ray C
na kusema ila anamuombea Mungu apone na arudi kwenye muziki kama zamani
kwani nafasi yake kwenye muziki bado ipo.
Ray C
“Leo hii kwenye muziki hatumuoni mtu kama Ray C, mpaka sasa hakuna
mtu kama Ray C hivyo chumba chake kwenye muziki bado kipo kinamsubiri
arudi tu.
Aliendelea “Sijakutana naye wala hatuongei ila namuombea Mungu kwani
tatizo lile ni kama maradhi mengine hivyo haliwezi kuisha kwa mara moja
linachukua muda, anahitaji maombezi na mimi namuombea kama navyojiombea
mimi nifanye kazi zikamilike tukutane kwenye show huko” alisema Lord
Eyes
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
❝BABU MWENYE NYUMBA❞ {♡Love Story♡_____Part..19} ∪₥ri_____+ ℳtunzi: ₲eofrey Mustafa, ₳rtist Jafa ✍ ℳaahali: Dar es salaam🇹🇿 ₩ha...
-
❝BABU MWENYE NYUMBA❞ {♡Love Story♡_____Part..29} ∪₥ri_____+ ℳtunzi: ₲eofrey Mustafa, ₳rtist Jafa ✍ ℳaahali: Dar es salaam🇹🇿 ₩ha...
-
❝BABU MWENYE NYUMBA❞ {♡Love Story♡_____Part..26} ∪₥ri_____+ ℳtunzi: ₲eofrey Mustafa, ₳rtist Jafa ✍ ℳaahali: Dar es salaam🇹🇿 ₩h...
No comments:
Post a Comment