Tuesday, November 8, 2016

Country Boy asema hawezi kufanya ‘Playback’, pia afunguka kuhusu tour yake ‘Dakika 45’ za Country Boy(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Rapa Country Boy amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amekua kisanaa hivyo hayuko tayari kufanya ‘Playback’ katika show zake na kwamba sasa anafanya muziki ‘live’ na band yake na ameamua kufanya hivyo kuwaonesha watu kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo.
Country Boy
Rapa Country Boy alisema hayo kupitia kipindi cha Bongo Fleva Top 20 ya East Africa Radio na kudai kuwa muziki wake sasa ni mkubwa hivyo haoni sababu ya kuendelea kufanya ‘Playback’ katika show hivyo sasa ni mwendo wa live music pamoja
na band yake.
Pia Country Boy amedai kuwa kwa sasa amenzisha ‘tour’ yake mwenyewe kuzunguka nchi nzima ambayo ameipa jina la ‘Dakika 45’ za Country Boy.
“Sasa hivi nimeanza tour yangu ya ‘Dakika 45’ za Country Boy nafanya live Music, live band, na watu wa Band nyuma, wapiga gitaa, wapiga Solo, Piano, watu wa Drums, kila mtu anafanya set up ya live show.
Aliendelea “hivyo kila nitakapokuwepo nitafanya live show na Band, ni kitu ambacho nataka nikifanye.
Hata ukiangalia wasanii wa Marekani
wanapofanya show wanafanya live mzee, mimi siwezi kufanya ‘playback’ wakati mimi ni msanii mkubwa ambaye nina uwezo wa kufanya vitu kibao.
Nataka kuwa prove watu kuwa nina uwezo
wa kufanya live lakini pia nataka kuwaonyesha energy ndiyo maana nimeweka dakika 45 za Country Boy sidhani kama kuna msanii yeyote anaweza kufanya show ya dakika 45 non-stop ya ngoma zake mwenyewe bila mtu mwingine mimi nimeamua kufanya hivyo”
alimalizia Country Boy

No comments:

Post a Comment