Saturday, February 25, 2017

ALI KIBA KUACHIA ALBUM (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Hatimaye Alikiba ameweka wazi jina la Album yake mpya inayotarajia kwenda kutoka mwaka huu.

Kupitia interview yake na TransAfricaRadio ya South Africa, Kiba amesema Album yake itaenda kwa jina la "DIARY_OF_ALIKIBA" na amechagua jina hilo sababu litabeba the whole of kiba.
Mbali na hilo, Kiba ametaja baadhi ya international artists watakaokuwa featured kwenye Album hiyo ikiwemo na Mama Yvonne Chakachaka, kundi la Micasamusic pamoja na wasanii wengine wa kimataifa atakokuja kuwataja hapo mbeleni.
Note That:
Diary Of Alikiba itakuwa ni Album ya tatu kwa Alikiba baada ya Album zake za awali #Sinderela ya 2008 na #Alllyk4Real ya 2010 ambapo Album yake ya pili iliweka rekodi ya aina yake kwa kuwa ya kwanza kwa mauzo East Africa, The most selling Album in East Africa.
Distribution ya Album hii itakuwa Worldwide kupitia Label yake ya SonyMusic kwa kutumia mfumo Digital platforms.

Mtoto wa Muhammad Ali apigwa chini Airport kisa dini yake(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Hali ya ubaguzi inaonekana kama inatambaa chini kwa chini huko nchini Marekani tangu Donald Trump kutangaza kupiga marufuku baadhi ya mataifa kuingia nchini Marekani.
Bad newz ni kwamba mtoto wa Muhammad Ali alikutana na vikwazo vikubwa wakati ametua katika uwanja wa ndege wa Florida na sababu kubwa mtoto huyo alicholalamika ni kwamba wamemzuia kisa dini yake ya Kiislamu.
Akiongea na mtandao wa Tmz, mzungumzaji wa mtoto wa Muhammad Ali jr, Chris Mancini amefunguka kwa kusema kwamba, Kijana wa Muhammed Ali alizuiliwa na watu wa uhamiaji wa Fort Lauderdale-Hollywood kwa masaa kibao baada ya trip yake na Mama yake huko Jamaica february 7, na ishu hiyo imekuja muda mchache tu tangu Jaji atupilie mbali uamuzi wa Trump kuhusu marufuku ya wahamiaji kuingia nchini.
Ishu nyingine ni kwamba mke wa Muhammed Ali, Khalilah Ali yeye alifanikiwa kupita kwenye uwanja wa ndege huo ila, Jr yeye alizuiliwa na kuingizwa kwenye chumba ambacho kila muda alikuwa akiulizwa maswali kama yeye ni Muislamu na jina lake hilo amelipata vipi, kitu hicho kilimuumiza sana Muhammed Ali Jr na kumlazimu kufungua kesi juu ya ishu hiyo.

WEMA SEPETU:SABABU ZA KUHAMIA CHADEMA (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Msanii wa filamu nchi Tanzania Wema Sepetu ametangaza rasmi kukihama Chama cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) siku moja moja baada ya taarifa hizo kusambaa kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania.
Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.
“Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA… Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana, kwa sasa I am a proud member of CHADEMA”. Amesema Wema Sepetu.

Friday, February 24, 2017

ROTA VS COUNTRY BOY AAAHH WAPI REMIX (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Bofya hapa https://www.hulkshare.com/yqo1agb5wveo kuskiliza AAHH WAPI ikiwa ni remix imefanywa na ROTA maarufu km FREESTYLE DOCTOR chini mtayarishaji ambae anakuja juu kwa sasa mjini MOROGORO Producer GS wa NON STOP MUSIC.Original ya wimbo huu amefanya COUNTRY BOY na producer ni S2 KIZZY.

TEGA SIKIO MSIKILIZE JAY FOX (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Bofya hapa https://www.hulkshare.com/rsfyoldpdwcg  kuskiliza wimbo wa Rapa JAY FOX uitwao TEGA SIKIO,
Studio PLAY BACK RECORD,
Producer MCHALLE,Tunduru-Ruvuma.
Cont +255752531687/+255789339863

FRIDAY NIGHT LIVE INA BEI YAKE LEO (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Hit maker wa BONGE LA TOTO na sasa BEI YAKE wakuitwa ELLISHA JAMES leo atatambulisha VIDEO ya wimbo wake uitwao BEI YAKE katika kituo cha television cha EATV kwenye kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE usiku wa leo.Audio imefanyika na DAZ NALEDGE,mastering ikafanywa na AMBROSE DUNGA,Video kafanya FREEMAN.

Thursday, February 23, 2017

MASOGANGE HATIANI, WEMA SEPETU KESI YAKE YAHAIRISHWA. (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Ripoti ya mkemia Mkuu wa serikali imethibitisha  Mwanamitindo Agnes Gerald  known as Masogange kuwa  ni mtumiaji wa  madawa ya kulevya aina ya heroine. Masogange ambaye alikamatwa kati ya tarehe 7 hadi 14 ya mwezi wa pili baada ya kuingia kuapishwa kwa kamshina wa Tume ya kudhibiti madawa ya kulevya nchini.
at the sametime mrembo Wema Sepetu  ambaye alihusishwa kwenye sekeke hilo la utumiaji wa madawa  ya kulevya  kesi yake  imehairishwa kutokana na upelelezi kutokukamilika hadi pale itakaposikilizwa tena Machi 15 Mwaka Huu.

MSANII CHINDO MAN AFIWA NA MTOTO WAKE.(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Msanii maarufu wa kundi la Watengwa Chindo Man a.k.a Umbwa anaefanya vizuri kwa sasa na wimbo wake wa TORATI YA MTAA amefiwa na mtoto wake wa kiume jijini London baada ya kuungua na moto taarifa zinasema wakati moto huo ukiwaka hakuwepo mtu karibu kutoa usaidizi! Km familia,ndugu na rafiki wa familia hii  tunapenda kutoa pole kwa Chindo Man pamoja na familia yake kwa kipindi hiki kigumu. #RipSon

Monday, February 20, 2017

Soulja Boy afunguka haya juu ya pambano lake la ngumi na Chris Brown (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Kwa Bongo kiki ikifanywa na staa yoyote huwa ni kitu cha ajabu sana lakini kumbuka mastaa wakubwa wa Marekani ndio mabingwa wa mambo hayo na wao ndio walioanzisha kwa ajili ya kujiweka juu kila siku.
Mkali Soulja boy amesema kuwa Chris Brown anamuogopa mno ndiyo maana ameshindwa kusign mkataba wa pambano la ngumi baina yao wawili ambalo limepewa air time kwa muda mrefu sasa
Soulja amesema hayo kupita ukurasa wake wa mtandao wa twitter na kudai kuwa Chris asimpigie simu tena kuhusu mambo ya wanawake kwakua ni muoga kupita kiasi.

Hizi hapa Tweets za Soulja Boy

Soulja na Chris Brown walianza kulumbana miezi kadhaa iliyopita baada ya mrembo Karruche Train kupost picha kwenye Mtandao wa Instagram na Sou’ja kulike kitu kilichoonekana kumkosesha raha Chris.

Alichoandika Shamsa Ford kuhusu Mumewe Chidi Mapenzi (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea mitandaoni naamini utakuwa unafahamu kuwa mume halali wa muigizaji Shamsa Ford anayefahamika kama Chidi Mapenzi ni mmoja kati ya watu ambao wamepitiwa na sakata la Madawa ya Kulevya nchini.
Na inavyosemekana ni kwamba hadi sasa mfanyabiashara huyo maarufu wa nguo jijini Dar es Salaam bado anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kama anajihusisha na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya.
Mwanadada Shamsa Ford ameendelea kuonyesha mapenzi yake ya dhati kwa mumewe huyo na kudai kwamba hajutii kuolewa na yeye bila kujali matatizo yote yanayo wakumba sasa hivi bali anaamini ni mitihani ya Mungu tu.
Ujumbe ambao ulisomeka kama “nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani inshaallah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..”
Mungu amjaze roho hiyo hiyo ya uvumilivu mwanadada Shamsa Ford ili waweze kudumu katika maisha yao ya ndoa na mumewe huyo Rashid.

Cassper Nyovest adai hakuna Rapa mkali zaidi yake Barani Africa(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Ule ushindani baina ya rappers wa Afrika Kusini AKA na Cassper Nyovest bado ni shidaa!! yani nikisema niwaulize wadau wa muziki wa Hip Hop kuwa kati ya AKA na Cassper Nyovest nani mkali zaidi, tutabishana sana na wala hatutayamaliza.
Cassper Nyovest kwa upande mwingine ana mtazamo wa tofauti kabisa, yeye anaamini kuwa ‘hakuna rappa mkali’ barani Africa zaidi yake!
Kwenye interview aliyofanya hivi karibuni nchini South Africa na kipindi cha Slikour On Life, Cassper alidai kuwa anaamini hakuna mkali zaidi yake kwenye game nzima ya Hip Hop.
Cassper Nyovest
Nenda Marekani uwaulize kuhusu Hip Hop ya Africa, watakutajia jina moja tu na hiyo ni kwasababu ya vitu nilivyovifanya hapa, kuperform na kujaza ukumbi wa The Dome, Orlando Stadium, na vitu vingine vikubwa kama hivyo…”. Alisema Cassper Nyovest.
Aliendelea kufunguka na kusema kuwa hafikiri wala hana mipango yoyote ya kuondoka Africa… “Nafanya hivi vyote kutoka huku. Mfumo wangu umebadilika. Ni bora kubadilisha game kutoka nyumbani. Mimi ni msanii kubwa wa Hip Hop kwa Africa so kwanini nisifanye ninachokifanya kwa ubora zaidi huku huku? Wananijua mimi kwa ukubwa wangu Africa”. Cassper Nyovest.
Wawili hao waliripotiwa kumaliza bifu yao baada ya AKA kwenda kumpongeza hasimu wake, Cassper kwenye show yake ya kihistoria mwaka jana, mwezi oktoba, aliyomshuhudia akiweka historia kubwa ya kuwa msanii wa kwanza wa hip hop kutoka nchini humo kuujaza uwanja wa mpira wa Orlando jijini Johannesburg.

Nikki wa Pili awachana wasanii wenye mawazo haya juu ya Kundi la weusi (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Rapper na mwanazuoni Nikki wa Pili, amefunguka kwa kutoa ujumbe unao walenga moja kwa moja Wasanii wenye mawazo ya kwamba, Wasanii kutoka kwenye kundi la Weusi wanabebwa na Media.
Rapper huyo wa Kundi la Weusi amedai kuanzia mwezi Januari mpaka sasa ana nyimbo 10 ambazo zipo tayari na G-Nako nae ana zaidi ya nyimbo 20 kitu ambacho anaamini ndiyo kinawafanya hao kuwa bora kila kukicha na sio kama mawazo ya baadhi ya Wasanii wanao dhani kuwa wanabebwa ile hali hawafanyi kazi kwa bidii kama wao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikki alipost ujumbe huu..
“January mpaka sasa nimesharekodi zaidi ya nyimbo 10 @gnakowarawara amerekodi zaidi ya nyimbo 20 labda ndio sababu nakaribia kufikisha miaka 10 kwenye game…. hainabahati/wala kubebwa… fanya kazi.. “Ameandika Nikki wa Pili kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo mkali huyo wa hit ya Sweet Mangi ametumia fursa hiyo pia kuutarifu Umma kuwa wiki lijalo G-Nako anaachia mkwaju wake mpya kwa kuandika “New muzik toka kwa @gnakowarawara Wiki Ijayo…….weusi News”.
Moja kati ya wasanii ambao walishawahi kukiri wazi kuwa Weusi wanabebwa na Media ni Young Killer kupitia wimbo wake wa ‘Sinaga Swaga’ na wimbo mwingine mpya wa Nay wa Mitego ambao ni gumzo kwa sasa ‘Muda wetu’.
Ingawaje Nay wa Mitego hajataja msanii yeyote mpaka sasa anaebebwa ila alisema ipo siku atawataja. Moja ya mastari kwenye ngoma hiyo anasema “Wanabebwa kwa upepo wa promotion”.

Thursday, February 2, 2017

Harmorapa amkosha P Funk kwa kitendo hiki(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Producer mkongwe na mwenye heshima yake P Funk Majani ameibuka na kumzungumzia huku akimsifia msanii anayeibukia kwa kasi katika bongo fleva, Harmorapa na kusema kuwa rapa huyo ni “level nyingine”.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na picha mbalimbali za Harmorapa mitandaoni zikimuonesha akiwa ameshikilia pesa nyingi jambo ambalo limemfanya producer huyo kuibuka na kumwagia misifa.
“Chezea Harmorapa wewe!!! Levo zingine hizi” alindika P Funk Majani kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Tangu Msanii Harmorapa ameingia kwenye muziki kwa kuanza kujifafanisha na msanii Harmonize, kila wakati rapa huyo amekuwa akiingia kwenye ‘headline’ mbalimbali na kuzungumziwa na wasanii wengi wakubwa nchini, wengine wakifurahishwa na matendo yake huku wengine wakimdhihaki na kuona kuwa hastaili kuwa mwanamuziki.

Hackers wadukua radio na kucheza ngoma ya YG ‘F*ck Donald Trump’ (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Mambo yanazidi kunuka huko nchini Marekani na safari hii Wadukuzi wamedukua stesheni za radio na kucheza wimbo wa “F*ck Donald Trump”
Uamuzi wa Trump juu ya waislamu bado imekuwa ni hali mbaya, Sasa Wadukuzi wameamua kuvamia stesheni zote ndogo ndogo za radio na kuzidukua kwa kucheza ngoma ya YG ya “F*ck Donald Trump” kwa muda wa dakika 20.
Kupitia taarifa ambayo imetolewa na kituo cha radio cha Salem, SC, waliamua kufnguka juu ya udukuzi huo wa radio hizo na kuwaomba radhi mashabiki juu ya tukio ambalo lilitokea kwa dakika 20 na kufanikiwa kulizima tatizo hilo.