Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na
picha mbalimbali za Harmorapa mitandaoni zikimuonesha akiwa ameshikilia
pesa nyingi jambo ambalo limemfanya producer huyo kuibuka na kumwagia
misifa.
“Chezea Harmorapa wewe!!! Levo zingine hizi” alindika P Funk Majani kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Tangu Msanii Harmorapa ameingia kwenye muziki kwa kuanza kujifafanisha
na msanii Harmonize, kila wakati rapa huyo amekuwa akiingia kwenye ‘headline’
mbalimbali na kuzungumziwa na wasanii wengi wakubwa nchini, wengine
wakifurahishwa na matendo yake huku wengine wakimdhihaki na kuona kuwa
hastaili kuwa mwanamuziki.
No comments:
Post a Comment