Rapper huyo wa Kundi la Weusi amedai kuanzia mwezi Januari mpaka sasa ana nyimbo 10 ambazo zipo tayari na G-Nako nae ana zaidi ya nyimbo 20 kitu ambacho anaamini ndiyo kinawafanya hao kuwa bora kila kukicha na sio kama mawazo ya baadhi ya Wasanii wanao dhani kuwa wanabebwa ile hali hawafanyi kazi kwa bidii kama wao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikki alipost ujumbe huu..
“January mpaka sasa nimesharekodi zaidi ya nyimbo 10
@gnakowarawara amerekodi zaidi ya nyimbo 20 labda ndio sababu nakaribia
kufikisha miaka 10 kwenye game…. hainabahati/wala kubebwa… fanya kazi.. “Ameandika Nikki wa Pili kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo mkali huyo wa hit ya Sweet Mangi ametumia fursa hiyo pia
kuutarifu Umma kuwa wiki lijalo G-Nako anaachia mkwaju wake mpya kwa
kuandika “New muzik toka kwa @gnakowarawara Wiki Ijayo…….weusi News”.Moja kati ya wasanii ambao walishawahi kukiri wazi kuwa Weusi wanabebwa na Media ni Young Killer kupitia wimbo wake wa ‘Sinaga Swaga’ na wimbo mwingine mpya wa Nay wa Mitego ambao ni gumzo kwa sasa ‘Muda wetu’.
Ingawaje Nay wa Mitego hajataja msanii yeyote mpaka sasa anaebebwa ila alisema ipo siku atawataja. Moja ya mastari kwenye ngoma hiyo anasema “Wanabebwa kwa upepo wa promotion”.
No comments:
Post a Comment