Cassper Nyovest kwa upande mwingine ana mtazamo wa tofauti kabisa, yeye anaamini kuwa ‘hakuna rappa mkali’ barani Africa zaidi yake!
Kwenye interview aliyofanya hivi karibuni nchini South Africa na kipindi cha Slikour On Life, Cassper alidai kuwa anaamini hakuna mkali zaidi yake kwenye game nzima ya Hip Hop.
Cassper Nyovest
“Nenda Marekani uwaulize kuhusu Hip Hop ya Africa,
watakutajia jina moja tu na hiyo ni kwasababu ya vitu nilivyovifanya
hapa, kuperform na kujaza ukumbi wa The Dome, Orlando Stadium, na vitu
vingine vikubwa kama hivyo…”. Alisema Cassper Nyovest.Aliendelea kufunguka na kusema kuwa hafikiri wala hana mipango yoyote ya kuondoka Africa… “Nafanya hivi vyote kutoka huku. Mfumo wangu umebadilika. Ni bora kubadilisha game kutoka nyumbani. Mimi ni msanii kubwa wa Hip Hop kwa Africa so kwanini nisifanye ninachokifanya kwa ubora zaidi huku huku? Wananijua mimi kwa ukubwa wangu Africa”. Cassper Nyovest.
Wawili hao waliripotiwa kumaliza bifu yao baada ya AKA kwenda kumpongeza hasimu wake, Cassper kwenye show yake ya kihistoria mwaka jana, mwezi oktoba, aliyomshuhudia akiweka historia kubwa ya kuwa msanii wa kwanza wa hip hop kutoka nchini humo kuujaza uwanja wa mpira wa Orlando jijini Johannesburg.
No comments:
Post a Comment