Monday, February 20, 2017

Alichoandika Shamsa Ford kuhusu Mumewe Chidi Mapenzi (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea mitandaoni naamini utakuwa unafahamu kuwa mume halali wa muigizaji Shamsa Ford anayefahamika kama Chidi Mapenzi ni mmoja kati ya watu ambao wamepitiwa na sakata la Madawa ya Kulevya nchini.
Na inavyosemekana ni kwamba hadi sasa mfanyabiashara huyo maarufu wa nguo jijini Dar es Salaam bado anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kama anajihusisha na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya.
Mwanadada Shamsa Ford ameendelea kuonyesha mapenzi yake ya dhati kwa mumewe huyo na kudai kwamba hajutii kuolewa na yeye bila kujali matatizo yote yanayo wakumba sasa hivi bali anaamini ni mitihani ya Mungu tu.
Ujumbe ambao ulisomeka kama “nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani inshaallah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..”
Mungu amjaze roho hiyo hiyo ya uvumilivu mwanadada Shamsa Ford ili waweze kudumu katika maisha yao ya ndoa na mumewe huyo Rashid.

No comments:

Post a Comment