Monday, February 20, 2017

Soulja Boy afunguka haya juu ya pambano lake la ngumi na Chris Brown (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Kwa Bongo kiki ikifanywa na staa yoyote huwa ni kitu cha ajabu sana lakini kumbuka mastaa wakubwa wa Marekani ndio mabingwa wa mambo hayo na wao ndio walioanzisha kwa ajili ya kujiweka juu kila siku.
Mkali Soulja boy amesema kuwa Chris Brown anamuogopa mno ndiyo maana ameshindwa kusign mkataba wa pambano la ngumi baina yao wawili ambalo limepewa air time kwa muda mrefu sasa
Soulja amesema hayo kupita ukurasa wake wa mtandao wa twitter na kudai kuwa Chris asimpigie simu tena kuhusu mambo ya wanawake kwakua ni muoga kupita kiasi.

Hizi hapa Tweets za Soulja Boy

Soulja na Chris Brown walianza kulumbana miezi kadhaa iliyopita baada ya mrembo Karruche Train kupost picha kwenye Mtandao wa Instagram na Sou’ja kulike kitu kilichoonekana kumkosesha raha Chris.

No comments:

Post a Comment