Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania.
Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya
kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali
visiwani Zanzibar.
“Kuanzia sasa mimi siyo tena
mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya
CHADEMA… Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania
demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi
kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti
ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu
sana, kwa sasa I am a proud member of CHADEMA”. Amesema Wema Sepetu.
No comments:
Post a Comment