Hali ya ubaguzi inaonekana kama inatambaa chini kwa chini huko nchini Marekani tangu Donald Trump kutangaza kupiga marufuku baadhi ya mataifa kuingia nchini Marekani.
Bad newz ni kwamba mtoto wa Muhammad Ali alikutana na vikwazo vikubwa wakati ametua katika uwanja wa ndege wa Florida na sababu kubwa mtoto huyo alicholalamika ni kwamba wamemzuia kisa dini yake ya Kiislamu.
Akiongea na mtandao wa Tmz, mzungumzaji wa mtoto wa Muhammad Ali jr, Chris Mancini amefunguka kwa kusema kwamba, Kijana wa Muhammed Ali alizuiliwa na watu wa uhamiaji wa Fort Lauderdale-Hollywood kwa masaa kibao baada ya trip yake na Mama yake huko Jamaica february 7, na ishu hiyo imekuja muda mchache tu tangu Jaji atupilie mbali uamuzi wa Trump kuhusu marufuku ya wahamiaji kuingia nchini.
Ishu nyingine ni kwamba mke wa Muhammed Ali, Khalilah Ali yeye alifanikiwa kupita kwenye uwanja wa ndege huo ila, Jr yeye alizuiliwa na kuingizwa kwenye chumba ambacho kila muda alikuwa akiulizwa maswali kama yeye ni Muislamu na jina lake hilo amelipata vipi, kitu hicho kilimuumiza sana Muhammed Ali Jr na kumlazimu kufungua kesi juu ya ishu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
❝BABU MWENYE NYUMBA❞ {♡Love Story♡_____Part..19} ∪₥ri_____+ ℳtunzi: ₲eofrey Mustafa, ₳rtist Jafa ✍ ℳaahali: Dar es salaam🇹🇿 ₩ha...
-
❝BABU MWENYE NYUMBA❞ {♡Love Story♡_____Part..29} ∪₥ri_____+ ℳtunzi: ₲eofrey Mustafa, ₳rtist Jafa ✍ ℳaahali: Dar es salaam🇹🇿 ₩ha...
-
❝BABU MWENYE NYUMBA❞ {♡Love Story♡_____Part..26} ∪₥ri_____+ ℳtunzi: ₲eofrey Mustafa, ₳rtist Jafa ✍ ℳaahali: Dar es salaam🇹🇿 ₩h...
No comments:
Post a Comment