Tuesday, July 18, 2017

NEW AUDIO[BOUMAN PROO ft JITI FLOW,ZILL VEGA]-MAMBO MENGINE BAADAE-

Click here https://my.notjustok.com/track/245817/mambo-mengine-badae to Download/listen MAMBO MENGINE BAADAE

French Montana anazidi kutengeneza heshima kwa Ghetto Kids

Moyo wa subira na juhudi ndio kitu kikubwa naweza nikakisema ambacho kimewafikisha hapa walipo sasa Ghetto Kids.
Tangu kuanza kwa safari yao ya kucheza kwenye matope mpaka kufika katika moja ya steji kubwa za kimataifa na kutumbuiza mbele ya umati mzito wenye macho ya wasanii wakubwa na watu mashuhuri Duniani, Hii ni moja ya blessing kubwa ambayo rapper French Montana ndio amekuwa kama ngazi kwa hawa madogo kuweza kusikika Duniani na kutolewa kwenye majarida makubwa kama “VIBE”.
Sasa nikusanue tu kwamba Madogo hao “GHETTO KIDS” kutoka Uganda, ambao walipata nafasi ya kushine na mnyamwezi French Montana kuanzia kwenye kichupa cha “Unforgettable” mpaka kwenye ukumbi wa tuzo za BET sio kazi ndogo.
Kupitia Jarida la VIBE, French Montana alifunguka kwa kuzitaja gharama ambazo alitumia kuwasafirisha madogo hao kutoka Uganda mpaka Marekani ambapo alisema alitumia takribani kama dola 100,000, Stori haikuishia hapo Good Thing ni kwamba French amepanga kuwatumia madogo hao katika Tour yake ambayo atashirikiana na The Weeknd kwa ajili ya kuonekana Zaidi Ulimwenguni.

Skendo ya Wolper iliyomuumiza zaidi Harmonize

Hakuna asiyefahamu kwamba miezi michache iliyopita Entertainment Industry hapa Bongo ilikuwa ikiambatana na couple ya mastaa wawili kutoka katika nyanja tofauti tofauti katika wigo wa Entertainment.
Mmoja kutoka Bongo Flevani ambaye ni Harmonize wa WCB na kutoka Bongo Movie ni mrembo Jacqueline Wolper ambao kwa hivi sasa kila mmoja anaendelea na mahusiano mapya baada ya kuvunjika kwa uhusiano wao.
Ikiwa inajulikana mastaa hao ni watu wa skendo kila kukicha, jana July 17 Harmonize ameshare na sisi story kuhusu skendo ambayo ilimuumiza zaidi katika mahusiano yake na Wolper.
Kupitia Amplifaya ya Clouds fm Harmonize ametusanua kuwa skendo ya Jacqueline Wolper kurecordiwa video akiwa mtupu na aliyekuwa mpenzi wake kipindi cha nyuma ni kitu ambaccho kilimuumiza sana na kumfanya afikirie itakuwa vipi endapo video hiyo ikivuja.
Katika hali ya kimapenzi Harmonize amedai kuwa alikuwa akijipa moyo juu ya hilo ukizingatia mpenzi wake huyo sio mtu wa kwanza kutokewa na jambo kama hilo, akitolea mfano mastaa wakubwa Duniani kama Kim Kardashian, Ammber Rose ni watu ambao wamewahi kukumbwa na skendo kama hizo na maisha yakaendelea.

Billnass anatamani kuzifanyia Remix Ngoma za Godzilla

Ikiwa kumekuwa na story kitaani za kudai kwamba Billnass ndiye aliyeziba pengo la Godzilla kwenye game ya music baada ya kupotea, ila personally Billnass hakubaliani na story hizo kwasababu anadai kuamini kuwa hawezi ziba pengo la mtu ambaye hajafa.
Billnass ametusanua kuwa Zilla ni rapper mkali na anayestahili heshima kubwa kutokana na yeye kumtangulia kwenye game na zipo ngoma zake ambazo anazikubali kinoma kias kwamba huwa anatamani hata kuzifanyia remix.
Billnass amezitaja Nataka na King Zilla kama ngoma flani hivi kali kutoka kwa Godzilla na anazikubali kinoma kias kwamba huwa anatamani hata kuzifanyia remix.

Saturday, July 15, 2017

“TAREHE 26 AUGUST ITAKUWA NI KIFO AU KUFA” HAYA NDIO MANENO YA MAYWEATHER KWA MCGREGOR

Bondia mwenye mbwembwe na asiyewahi kupoteza hata mchezo mmoja kati ya 50 aliyocheza nchini wingereza ametoa tamko kali kwa mpinzani wake wa karibu ambaye anakwenda kupigana nae siku ya tarehe 26 mwezi ujao katika ukumbi wa T-mobile Arena jijini La Vegas.
Mayweather amemwembia McGregor kuwa siku ya 26 itakuwa ni kifo ama kufa katika ukumbi wa T-Mobile Arena ameyasema hayo mbele ya McGregor ambaye naye hakuwa nyuma katika kuonyesha mbwembwe baada ya kumchezea Mayweather akionyesha kumdhihaki bondia huyo.
Sasa haya ndio matukio ambayo yametokea pale nchini Wingereza katika mkutano na waandishi wa habari.

SITAMBUI U-BOSS WA ALIKIBA KWENYE ROCKSTAR400-[BARAKAH DA PRINCE]

Siku chache zilizopita lebo ya muziki ya Rockstar 4000 ilimtambulisha mkali wa muziki nchini Alikiba kama mmoja wa viongozi katika body ya madirector katika lebo hiyo.
Alikiba na Viongozi wenzie Rockstar 4000


 Kwenye kipindi cha Ala za Roho ya Clouds fm Diva The Bawse alikuwa na Exclusive interview na Baraka Da Prince ambaye naye pia ni msanii kutoka chini ya uongozi wa Record Label hiyo.
Cha kushangaza ni pale Baraka Da Prince alipo kanusha kuzifahamu taarifa za Alikiba kupewa uongozi katika lebo hiyo na kudai kuwa hata yeye anaziona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii tu.
Baraka Da Prince amedai kuwa bado hajapewa taarifa kutoka katika uongozi wa juu kuwa Alikiba ni mmoja wa viongozi katika lebo hiyo, na hivyo hamtambui Alikiba kama kiongozi katika lebo hiyo.
Unaweza kuona ni kipi kinaendelea baina ya wakali hawa ikiwa hivi karibuni kumekuwa na story zinazo wahusisha kutokuwa na maelewano mazuri. Niachie comment yako kwa chochote ambacho umekielewa kuhusu wakali hawa.

Sunday, July 9, 2017

JAY Z NA 4:44 WACHAFUA ITUNES KENYA,UGANDA NA AFRICA KUSINI

Kwa maneno mafupi tu naweza nikakwambia kwamba rapper Jay-Z “Halichachi”, ndani ya masaa 24 baada ya kuachiwa kwenye mtandao wa Itunes album ya 4:44 inaongoza kwa kuwa namba moja katika jumla ya nchi 38.
4:44 ni moja ya Album ambayo imeteka attention kubwa ya mashabiki na wasanii na hyo ni kutokana na mistari kwenzi ambayo inapatikana humo ndani, sasa nchi ambazo Album hiyo imeshika nafasi ya kwanza katika mtandao wa Itunes ni United States, UK, Germany, Canada, Australia, Mexico, Denmark, Ireland, Norway, Switzerland, Russia, Sweden, South Africa, Finland, Poland, Malaysia, India, Panama, Sri Lanka, Anguilla, Antigua, Bahamas, Barbados, Bermuda, Botswana, Ghana, Indonesia, Israel, Kenya, Nigeria, Uganda, Trinidad na Tobago, Saudi Arabia, Mozambique, Lebanon, Saudi Arabia, Namibia na Zimbabwe.

GOOD NEWS KWA MASHABIKI WA MUZIKI WA ALI KIBA

Ni dhahiri kuwa ni muda mrefu umepita tangu mfalme wa muziki wa Bongo fleva Alikiba alipoachia ngoma kwa mara ya mwisho, ambapo wakali wa hizi mambo wanadai kuwa ni zaidi ya mwaka sasa tangu Alikiba alipoachia wimbo wake wa Aje ukiachilia mbaali ile remix ambayo ilifuata baadae.
Hali ambayo ilipelekea mashabiki wa Alikiba kuwa na kiu cha muda mrefu cha ngoma mpya kutoka kwa mkali huyo na kupelekea mambo mengi kuzungumzwa kitaani.
Good News ni kwamba Alikiba kupitia XXL ya Clouds fm ametusanua kuwa muda wowote kuanzia sasa ataachia ngoma mpya kwasababu ni ngoma nyingi ambazo amekwisha rekodi na zipo ndani tayari kwa kutoka.
Alikiba amedai kuwa time hii hatokuwa na haja ya kutangaza kabla ya kutoa ngoma mpya, atakachofanya ni kushusha magoma tu watu watakutana nayo hewani.
“Nyimbo yangu inatoka hivi karibuni, siwezi kusema ni lini ila ninachoweza kusema tu ni hivi karibuni. Sasa hivi nataka tu ni-surprise sababu sifanyi hata teaser, itatoka tu.” Alisema Alikiba.
Pia Alikiba aitusanua kuwa ngoma yake inayofuata ni ngoma ambayo atakuwa amefanya yeye peke yake na wala hajamshirikisha mtu yeyote yule kutokana na mashabiki zake kuhitaji ngoma ya aina hiyo kwasababu hapa katikati aliachia ngoma kama Kajiandae ambayo yuko na Ommy Dimpoz, Nisamehe ambayo alishirikishwa na Baraka The Prince na hata Lini ya Navy Kenzo ila mashabiki zake bado walihitaji ngoma mpya.

NEW AUDIO[BELLE 9]-MFALME-

NEW AUDIO[G NAKO]-MADEKO-

NEW AUDIO[MAGA V]-CHUGA KAMA PARIS-

NEW AUDIO[RAYVANNY]-CHUMA ULETE-

NEW AUDIO[DIAMOND PLATINUM]-ENEKA-

NEW AUDIO[BARNABA,BILLNAS,OBRIZ]-KWAKO-