Sunday, July 9, 2017

GOOD NEWS KWA MASHABIKI WA MUZIKI WA ALI KIBA

Ni dhahiri kuwa ni muda mrefu umepita tangu mfalme wa muziki wa Bongo fleva Alikiba alipoachia ngoma kwa mara ya mwisho, ambapo wakali wa hizi mambo wanadai kuwa ni zaidi ya mwaka sasa tangu Alikiba alipoachia wimbo wake wa Aje ukiachilia mbaali ile remix ambayo ilifuata baadae.
Hali ambayo ilipelekea mashabiki wa Alikiba kuwa na kiu cha muda mrefu cha ngoma mpya kutoka kwa mkali huyo na kupelekea mambo mengi kuzungumzwa kitaani.
Good News ni kwamba Alikiba kupitia XXL ya Clouds fm ametusanua kuwa muda wowote kuanzia sasa ataachia ngoma mpya kwasababu ni ngoma nyingi ambazo amekwisha rekodi na zipo ndani tayari kwa kutoka.
Alikiba amedai kuwa time hii hatokuwa na haja ya kutangaza kabla ya kutoa ngoma mpya, atakachofanya ni kushusha magoma tu watu watakutana nayo hewani.
“Nyimbo yangu inatoka hivi karibuni, siwezi kusema ni lini ila ninachoweza kusema tu ni hivi karibuni. Sasa hivi nataka tu ni-surprise sababu sifanyi hata teaser, itatoka tu.” Alisema Alikiba.
Pia Alikiba aitusanua kuwa ngoma yake inayofuata ni ngoma ambayo atakuwa amefanya yeye peke yake na wala hajamshirikisha mtu yeyote yule kutokana na mashabiki zake kuhitaji ngoma ya aina hiyo kwasababu hapa katikati aliachia ngoma kama Kajiandae ambayo yuko na Ommy Dimpoz, Nisamehe ambayo alishirikishwa na Baraka The Prince na hata Lini ya Navy Kenzo ila mashabiki zake bado walihitaji ngoma mpya.

No comments:

Post a Comment