Moyo wa subira na juhudi ndio kitu kikubwa naweza nikakisema ambacho kimewafikisha hapa walipo sasa Ghetto Kids.
Tangu kuanza kwa safari yao ya kucheza kwenye matope mpaka kufika katika
moja ya steji kubwa za kimataifa na kutumbuiza mbele ya umati mzito
wenye macho ya wasanii wakubwa na watu mashuhuri Duniani, Hii ni moja ya
blessing kubwa ambayo rapper French Montana ndio amekuwa kama ngazi kwa hawa madogo kuweza kusikika Duniani na kutolewa kwenye majarida makubwa kama “VIBE”.
Sasa nikusanue tu kwamba Madogo hao “GHETTO KIDS” kutoka Uganda, ambao walipata nafasi ya kushine na mnyamwezi French Montana kuanzia kwenye kichupa cha “Unforgettable” mpaka kwenye ukumbi wa tuzo za BET sio kazi ndogo.Kupitia Jarida la VIBE, French Montana alifunguka kwa kuzitaja gharama ambazo alitumia kuwasafirisha madogo hao kutoka Uganda mpaka Marekani ambapo alisema alitumia takribani kama dola 100,000, Stori haikuishia hapo Good Thing ni kwamba French amepanga kuwatumia madogo hao katika Tour yake ambayo atashirikiana na The Weeknd kwa ajili ya kuonekana Zaidi Ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment