Thursday, February 25, 2016

Kharda the truth ft beka title milele [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]









Bofya hapa https://mkito.com/song/kharda-the-truth-ft-beka-title-milele/18746 kupakua wimbo wa Kharda the truth ft Beka title, wimbo umefanyika katika studio za DM RECORD. Kwa mawasiliano cheki na Kharda kwa nambari +255 764 869374.
Powered by www.babalaoinc.blogspot.com follow @babalaotv

JAMBO SQUAD.Official Video (DIGIDIGI) WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM

   















 Bofya hapa https://youtu.be/aKH2RtRxKBI kutazama video ya wimbo wa kwao Jambo Squad uitwao DIGI DIGI,Video imefanyika EMPIRE STATE wakati audio ikiwa imefanyika NOIZ MAKER.
       Powered by www.babalaoinc.blogspot.com @babalaotv

WE SO HIGH Young Eyez ft Rude Rodgers,Big JOOH,Tonny Trigger,Ram32,SnakeFire [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

                        Bofya hapa https://mkito.com/song/we-so-high/18967  kupakua wimbo wa Young Eyez uitwao WE SO HIGH aliofanya kwa producer Justinoo.Kwa mawasiliano cheki nae kwa nambari +255672453518.
           Powered by www.babalaoinc.blogspot.com @babalaotv

Wednesday, February 24, 2016

Top G-Penzi Langu [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA http://mdundo.com/dl/34657/low kupakua wimbo wa TOP G Swahili chini ya mkono wa Affection Music na kwa mahojiano/mawasiliano zaidi check na #TopG kwa Nambari +255 719 158 975 or 0765 755 084 powered by @vmgafrica @mkitodotcom www.vmgafrica.com  @defxtro #vmgafrica www.babalaoinc.blogspot.com @babalaotv #SupportYourOwn

ST Fupa-Sipati Picha (Mix.Noiz)[WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA https://mkito.com/song/sipati-picha/18814 kupakua ngoma ya ST Fupa toka Moshi ngoma kwa jina "Sipati Picha" na kwa mahojiano/mawasilano zaidi check na #STFupa kwa nambari +255 672 422 427 Powered by @vmgafrica @babalaotv @defxtro www.babalaoinc.blogspot.com #vmgafrica www.vmgafrica.com

Monday, February 22, 2016

Doca Man Ft G Bless Police Woman Official VideoWWW BABALAOINC BLOGSPOT...





Download

YOUNG EYEZ AJA NA WE SO HIGH [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

We so high ni wimbo uliofanyika katika studio za Cukaz Beat chini ya producer Justinoo,wimbo huo unamililikiwa na msanii mpya kabisa aitwae Young Eyez akiwa amewashirikisha wasanii wengine kadhaa kama Rude Rodgers Babalao (hit maker wa SITAKI SHARI) pia kuna Tonny Trigger,Big Jooh,Ram32 na Snake Fire.Chanzo chetu cha habari kilipiga story na Edwin Kahindi a.k.a Young Eyez na akatuambia kuna mengi yanakuja kwaio mashabiki wakae mkao wa kupokea mengi kutoka kwake.

Wednesday, February 17, 2016

JamboSquad-DigiDigi (NOIZ) [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA https://mkito.com/song/digi-digi/18840 Kupakua #DigiDigi by Manjeree Machalii ya Ara #JamBoSquad @chaliijambo @odiijambo Produced by @defxtro @noizmekah huku tukisubiri Official Video Directed by #EmpireStatemedia @Director_Nezar Wiki Ijayo kwa Mahojiano/mawasiliano zaidi check na @jambosquad kwa nambari au 0653 610 249 au 0762 164 241 Powered by @vmgafrica @defxtro www.babalaoinc.blogspot.com follow @babalaotv #vmgafrica #SupportUrOwn #LoveAfricanMusic

Monday, February 15, 2016

Pax Kweli ft Brown-Nahitaji (SamTimber) [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA https://mkito.com/song/turn-me-onnahitaji/18815 kupakua wimbo wa PaxKweli kwa jina "Turn Me On" Nahitaji na kwa mahojiano/mawasilano zaidi check nae kwa nambari +255 655 787 800 powered by @vmgafrica @mkitodotcom www.vmgafrica.com  @defxtro #vmgafrica www.babalaoinc.blogspot.com @babalaotv #SupportYourOwn

Saturday, February 13, 2016

AKA DIAMOND PLATINUMZ MAKE ME SING OFFICIAL VIDEO [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya hapa https://youtu.be/RzL6d7Q8qO0 kutazama video ya AKA na DIAMOND PLATINUMZ wimbo unaitwa MAKE ME SING

Yona Metallic ft Breeze-Rudi Nyumbani ['WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA https://mkito.com/song/rudi-nyumbani-ft-breeze/18731 kupakua wimbo wa Yona Metallic ft Breeze kwa jina "Rudi Nyumbani" na kwa mahojiano/mawasilano check nae kwa nambari
+255 765 569 856 powered by @vmgafrica @mkitodotcom www.vmgafrica.com  @defxtro www.babalaoinc.blogspot.com #vmgafrica @babalaotv #SupportYourOwn

Jimmy Jay wa Tams ft Disaster-Gifted (OPBeats)[WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA https://mkito.com/song/am-gifted/18478 kupakua wimbo wa Jimmy Jay wa Tams ft Disaster kwa jina "Gifted" produced by OP Beats na kwa mahojiano/mawasiliano zaidi check na Jimmy Jay kwa Nambari +255 768 435 461 powered by @vmgafrica @mkitodotcom www.vmgafrica.com  @defxtro www.babalaoinc.blogspot.com #vmgafrica @babalaotv #SupportYourOwn

Saturday, February 6, 2016

MeccaCheka-Kibantu (DeFatality) [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA https://mkito.com/song/kibantu/18679 kupakua wimbo #KIBANTU wa @mecca_chekatz #MeccaCheka @almandomwirora @rizzychaffu juu ya mdundo wa #DeFatality @mesenselektatz via @mkitodotcom  Powered by @vmgafrica @defxtro www.babalaoinc.blogspot.com  follow @babalaotv #vmgafrica #SupportUrOwn #LoveAfricanMusic www.vmgafrica.com

Jackal Family ft WiseMan-Bembea (NOIZ) [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA https://youtu.be/lMOAele7ut0 Kutazama #BEMBEA ya @jackalfamilytz @wiz_dady_jackal_family @a_white_jackal_family @wizboy_music ft @wisemantz Produced by @defxtro & Directed by @Director_Nezar #EmpireStatemedia na pia Bofya HAPA Kupakua Audio https://mkito.com/song/bembea/12667 Kwa Mahojiano zaidi chek na #JackalFamily Kwa nambari +255 788 134 613 au +255 689 091 906 Powered by @vmgafrica www.vmgafrica.com @defxtro www.babalaoinc.blogspot.com  follow @babalaotv #vmgafrica #SupportUrOwn #LoveAfricanMusic

Friday, February 5, 2016

Noizmekah Studios Ofa Ya Kurekodi [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

#SpecialOffer #DefLab @Noizmekah Production Studios kwa kurekodi Ngoma/audio kwa punguzo la bei Laki Na Nusu pamoja na Kusambaza/Publishing kupitia www.vmgafrica.com check na Producer DX @defxtro kwa nambari +255 715 240 005 au +255 757 611 860 Powered by #vmgafrica www.vmgafrica.com  @vmgafrica www.babalaoinc.blogspot.com @babalaotv #SupportYourOwn

Monday, February 1, 2016

KIBANTU ASILI YETU [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Pata Kionjo í ½í±í ¼í¿¾kisha Kaa mkao wa kuruka full ‪#‎KIBANTU‬ na @mecca_chekatz ‪#‎MeccaCheka‬ @almandomwirora @rizzychaffu juu ya mdundo wa ‪#‎DeFatality‬ @mesenselektatz Rasmi Ijumaa Tarehe 5 via @mkitodotcom https://mkito.com/artist-profile/mecca-cheka/666 Powered by @babalaotv @vmgafrica @defxtro follow ‪#‎vmgafrica‬ ‪#‎SupportUrOwn‬ ‪#‎LoveAfricanMusic‬ www.babalaoinc.blogspot.com #‎teamMeccaCheka

follow instagram page yetu @babalaotv

KcK-Fekeche Fekeche (Full Package) + LYRICS + BEAT [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Bofya HAPA https://mkito.com/song/fekeche-fekeche/18127 kupakua

KRIKINCHI KRAKANCHA LYRICS
Artist :kck supremacy
Track:fekeche fekeche
Studio:Noiz mekah prod.
Writtenby:spacdawg.atwn@ymail.com
VERSE 1 SPAC DAWG
Fekeche fekeche krikinchi krakancha,
Kwikwichi kwikwichi mchuchuu anakacha,
Krikinchi hii punch mbuchuchuu mbakacha,
Kifukuchu fukuchu krikinchi chuchu mkuchu jax,
Raff kibrooklyn krukuchuu crooklyn,
Fekeche fekeche prukuchuu church,
Bike yake cheche kudaka kicheche,
Krikinchi ndichi kufekeche feke,kwichi kwichi kwichi
Krokoncho chocho kupecha peke oga mavirokocho,
Kirikuu wa mapocho mletee ma dogydogy,
Hata kiforokocho kifo cha kokorochi,
Kumbonji ni kinky anataka double clickich
Krikinch krakancha

VERSE 2 BOOX

Fekeche fekeche krikinchi clutch
Click kichele besa trasa scratch
Mbele,switch krikinchi punch
Maushirodachi,sotohachijidachi
Nakaa shikodachi ni set lunch
Nikae musubidachi
Peleka wasanii kwa magetsadanii
Na Kwa getsadaichi
Ichi Née San Shi Go Rock Hach Sichi
Krikinchi pinchi ni tensi ya mjate
Krakancha Ten Atalokota ngada
Akose ya mkate fekeche fekeche
Shop akakate Anatwe ang'atwe
Afanywe kwikwichi kwikwichi
Krikinchi cheche

Chorus
Fekeche Fekeche krikinchi krakancha ,
Kwikwichi kwikwichi krikinchi krakancha,
Fekeche Fekeche krikinchi krakancha,
Kwikwichi kwikwichi krikinchi krakancha,
Fekeche fekeche krikinchi krakancha kwikwichi kwikwichi krikinch kra,
Fekeche fekeche krikinchi krakancha kwikwichi kwikwichi krikinchi kra,


follow our page on instagram @babalaotv
like our facebook page www.babalaoinc.blogspot.com


Drake amjibu Obama, ajifananisha na Jay Z na amemdiss tena MeekMill kwenye ‘Sumer sixteen’[WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Rapper kutoka toronto, Drake hataki hutani tena, amejibu watu wote kwenye wimbo wake mpya ‘Summer sixteen’
     Kuhusiana na suala la rais wa Marekani Barack Obama kudai kuwa Kendrick Lamar atashinda iwapo atashindanishwa na Drake kwa kuwa ana uwezo mkubwa zaidi wa kuandika mashairi ( Isome Hapa) Drake amejibu,
“Tell Obama that my verses is just like the whips that he in / The bullet proof,” amerap mwanzoni kabisa mwa wimbo huo.

Kwenye wimbo huo pia amedai zamani alikuwa anatamani kuwa chini ya Roc-A- Fella lakini sasa yeye ni sawa na Jay Z, Pia ametania kuhusiana na Swimming pool ya Kanye west
I used to wanna be on Roc-A-Fella then I turned into Jay/ Now I got a house in LA, Now I got a bigger pool than Ye/ And look man, Ye’s pool is nice, mine’s just big is what I’m saying
Amempondea rapper mwingine wa mji ambao anatokea yeye mwenyewe, Toronto,  Tory Lanez
“All you boys in the new Toronto want to be me a little,” Drake raps referring to fellow Toronto artist Tory Lanez.  “All your ex’s know I like my O’s with a V in the middle / You would love it if I went away or didn’t say nothing else / How am I keeping it real by keeping this shit to myself? / You was never gang, gang, gang, gang, you was never one of us / Had us fooled for a minute now we done all grown up / But I’m better off anyway, y’all never gon’ finish drake / Say you seeing ‘bout it when you see me man y’all never home anyway / Thought of things that you shoulda said, said things that you shouldn’t say / We even gave you the whole money play and ya’ll still broke to this day.”

Hajamuacha adui yake mkubwa kwasasa, Meek Mill, Drake alikuwa hajajibu chochote tangu Meek Mill aachie disstrack mbili kwenda kwake,
“I let the diss record drop you were standing right below me, nigga,” Drizzy raps. “We must have played it a hundred times, you was going to bed / Why would I put on a vest I expect you to aim for the head? / I coulda killed you the first time / You don’t have to try to say it louder nigga / We could hear you the first time / It’s nothing personal I would have done it to anyone.” 
Powered by @babalaotv www.babalaoinc.blogspot.com

Diamond amueka Rich Mavoko chini yake Wasafi ‘WCB’[WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM

Rich mavoko mara ya mwisho nilikuwa natakiwa nimsaini wasafi, Rich mavoko alitakiwa awe signed wasafi kabla ya nyimbo yake hii kutoka, ilitakiwa ikitaka awe chini ya wasafi, lakini kuna vitu vilichelewesha kwasababu kulikuwa na project namalizia kwanza,” Diamond aliiambia Ayo Tv  “Nikamwambia, alikuwa anazungumza na uongozi wangu, kwahiyo wakamwambia kwasababu ishafika time unatakiwa utoe wimbo basi itoe tu hii nyimbo alafu then after hapo ikiwezekana kuanzia next project ndo anaweza akawa anatoa nyimbo akiwa chini ya wasafi.” Alielezea.
    Hadi sasa waanii ambao wapo chini ya label hiyo ni pamoja na Harmonize na Raymond.
Powered by @babalaoTV www.babalaoinc.blogspot.com

RAPPER WAKAZI KUTOKA TANZANIA AWANIA “KORA AWARDS” NAMIBIA [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Rapper Wakazi kutoka hapa home Tz ambaye ni mkali kwenye anga za muziki wa Hip Hop ameingia kwenye Kinyang’anyiro cha kuwania tuzo “Kora_Awards ” ya Best Hip Hop Act 2016,  Tuzo ambazo zinategemea kutolewa March 20th huko Windhoek, Namibia.

Best Hip Hop Act 2016, Awards Nominees

Sarkodie (Ghana)
Stanley Enow (Cameron)
KO (South Africa)
Kiff No Beat (Ivory Coast)
Hamzaoui Med Amine (Tunisia)
Wakazi (Tanzania)
Hata hivyo kutoka Tanzania hatakuwa pekeyake bali, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Yamoto Band na Mrisho Mpoto, pia ni wasanii ambao wanawania tuzo siku hiyo.
Kuhusiana na ushidi Rapper “Wakazi” amesema kuwa  “Kuwa nominated tayari kwangu ni ushindi tosha!! Nimekuwa nafanya Muziki officially kwa kama 4 years now na sijawahi kuwa nominated Tuzo yoyote ile hata mara Moja. So nomination hii ina maana kubwa sana kwangu na ukichukulia pia ni Tuzo Za kimataifa. Nikishinda nitafurahi ila haimaanishi kuwa nitakasirika nisiposhinda. Coz kuchaguliwa kwangu naweza kusema ni kutokana na ubora wa Kazi zangu, consistency Pamoja na support Ya mashabiki ambayo ndio iliyoweza kufanya nionekane.”
Hivyo kwa wadau wa muziki make sure that unaonesha support yako ya kutosha ili kuhakikisha  Rapper “Wakazi” anaibuka mshindi na kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia Muziki wetu wa Hip Hop. Umoja ni nguvu, Utengani ni udhaifu. Ili ashinde Please Send “Kora 123″ to +248984000 to vote for Wakazi (@Wakazimusic) as the #BestHipHopAct in 2016 @Kora_Awards.  Cheers 2016.
Powered by @babalaoTV www.babalaoinc.blogspot.com

JAY MOE NA HILI GAME [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Sehemu ya pili
______________________
Neno "mocumentary" ambalo linabeba jina la album yake ya tatu, ambalo Jay Moe hulitamka kama "mokyumenari" limetokana na muunganiko wa maneno Jay Moe na Documentary. Utaratibu huu wa kuunganisha maneno wanamofolojia wa kiingereza huuita "Blending" ambapo sehemu ya neno moja huunganishwa na sehemu ya neno lingine kutengeneza neno jipya. Kwenye neno Jay moe amechukua Mo na kwenye neno Documentary amechukua Cumentary, akayaunganisha ikawa mocumentary. Kwa maneno rahisi waweza sema "Mocumentary" ni Documentary za jay moe au Makala za Juma Mchopanga.
Jay moe anatukumbusha kwamba yupo katika game kabla ukumbi wa Diamond Jubilee haujaanza kujazwa kwa maonesho ya wasanii mwanzoni mwa miaka ya 2000. Diamond Jubilee kwa mara ya kwanza ilijazwa na Juma Nature katika uzinduzi wa album ya Ugali mwaka 2003 (Mkoloni, 2016). Mdau mmoja alishawahi kusema "Juma Nature ni msanii pekee aliyewahi kuijaza diamond jubilee mara tatu na watu wakakosa pakukanyaga". Leo hii msanii kuujaza ukumbi mdogo tu wa maisha club, billz n.k anaandaa msululu wa wasanii ili kumpa sapoti kwenye shoo yake na bado ukumbi unaweza usijae.
Ukiacha Juma Nature Diamond jubilee iliwahi kujazwa wasanii wengine kama Profesa Jay, Daz nundaz, Gangwe Mobb, Dully sykes na T.I.D katika uzinduzi wa pamoja wa albam zao n.k (Ngwesa & Palla, 2016).
Ni enzi hizo pia Jay moe anasema nyimbo zilikuwa hazirekodiwi kwa kompyuta katika studio nyingi kama sasa. G solo katika kitabu chake kiitwacho harakati za Bongo Fleva anasema kwamba “Studio za kwanza ambazo zilikuwa ni analogy (analojia) zilimikiwa na watu binafsi waliokuwa ndugu na zilikuwa eneo la Magomeni Mikumi na zote zilikuwa katika nyumba moja. Wamiliki hao ambao ni Paul Muuto na mdogo wake Gerry Gumbo. Walikuja kuziuza studio hizo kwa taasisi za Don Bosco ndipo ikazaliwa Don Bosco Studio mwaka 1992. Mnamo mwaka 1994 studio ya mawingu ilianza kazi rasmi…. Mwaka 1998 MJ records ilianzishwa ikimilikiwa na Master J... studio moja tu ndiyo ilitumia mfumo wa digital (dijitali) ambayo ni sound crafters. Bei za kurekodi studio za analogy ilikuwa ni Shilingi 8,000 na kwenye studio zilizokuwa digital ilikuwa shilingi 25,000” (Mwanjoka, 2011).
Wakati Jay Moe anaingia katika ulingo wa muziki wa Tanzania, ni wakati ambao muziki wa Tanzania ulikuwa umetawaliwa na muziki wa Taarabu na Dansi/Bolingo na ndio ulikuwa ukipewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari kuliko muziki wa kizazi kipya. Wenye kumbukumbu nzuri mtakumbuka katika kipindi hicho kuelekea mwishoni mwa miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 ndipo kulikuwa na ushindani katika muziki wa Taarabu kati ya Khadija Kopa na Nasma Khamis Kidogo hali iliyepelekea kuanzia mtindo wa “mipasho” katika muziki wa taarabu kutokana na kutupiana vijembe katika nyimbo.
Ikumbukwe nyakati hizi ndizo nyimbo maarufu kama ‘Mambo iko huku”, “Sanamu la Michelin” za Nasma Kidogo, “Kinyago cha Mpapure” ya Mwanahawa Ally n.k zilikuwa zimeshika chati hali iliyofanya baadhi ya waimbaji taarabu kushirikishwa na wanamuziki wa kizazi kipya kwa mfano marehemu Nasma aliwahi kushikishwa katika kibao cha Gangwe Mobb kiitwacho wape Vidonge vyao. Abdul misambano pia alishawahi kushirikishwa kuimba kiitikio cha ‘asu’.
Katika muziki wa dansi, hiki kilikuwa kipindi ambacho bendi ya African Stars ama Twanga Pepeta ilikuwa katika ubora wake bila kuwasahau Tamtam, TOT, Wajelajela (ndanda Kosovo), Msondo Ngoma n.k walikuwepo pia katika chati. Twanga pepeta ilitawala muziki wa Tanzania kwa vipindi vikuu viwili kwa kipindi hicho; wakati safu ya uimbaji ikiongozwa na Banza stone aliyejiunga na Twanga mwaka 1995 na kutamba na nyimbo kama “kisa cha mpemba” n.k. Banza alipoondoka twanga mwaka 2001, Ally choki akashika usukani na kutamba na vibao kama ‘Jirani’, ‘chuki binafsi’ n.k. Upande mwingine Muumini mwinjuma alikuwa yuko moto na bendi ya Tamtam huku akipata umaarufu na kibao chake cha “Tunda”.
Kipindi hiki pia utaona waimbaji wa muziki wa dansi walianza kushirikishwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya. Wenye kumbukumbu mnaukumbuka wimbo wa “Achana nao” wa Mad Brain na Sister P wakimshirisha Ally Choki kuimba kiitikio cha wimbo huo. Tusiusahau pia wimbo wa “Msafiri” wa Kwanza Unit ambao walimshirikisha mzee wetu King Kikii (Mzee sugu au mzee wa kitambaa cheupe), “Hapo zamani” ya Sugu ft King Kiki na Kuna msanii (Nimemsahau jina) aliwahi kutumia kiitikio cha “Napenda Nipate lau nafasi” ya Kilwa Jazz Band. Huu wimbo wa msafiri humo ndani King Kikii hakushirikishwa tu bali Master Jay (mtayarishaji wa kibao hicho) alisampo kibao hicho pia. Kuna uwezekano hiki kikawa ndio kibao cha kwanza cha muziki wa dansi Tanzania kusampuliwa na watayarishaji wa muziki wa kizazi kipya.
Asha Baraka, mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta anakubaliana na Jay Moe anaposema kwamba mziki wa kizazi ndio chanzo cha kufa (kuzorota) kwa taarabu na bolingo (dansi). Katika mahojiano na Gazeti la Mwananchi aliwahi kunukuliwa akisema ukuaji wa muziki wa kizazi kipya umeathiri soko la dansi. Anasema mwanzoni mwitikio ulikuwa mkubwa kuliko sasa hata mchango wa vyombo vya habari umepungua upande wa kupiga nyimbo za dansi hewani (Matandiko, 2014).
Itaendelea...........
Imeandikwa na
MALLE HANZI
0715076444
©2016
Powered by @babalaoTV www.babalaoinc.blogspot.com

JAY MOE NA HILI GAME [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Sehemu ya kwanza
______________________
Katikati mwa Miaka ya 2000 kituo cha Luninga cha EATV ama Channel 5 kilikuwa na kipindi kinachoitwa "In da House". Kipindi hicho kilikuwa hakina mtangazaji maalumu ila kilikuwa na kawaida ya kumualika msanii ambaye hugeuka mtangazaji na pia kuchagua nyimbo anazozipenda.
Kuna kipindi alichaguliwa Kala Pina kuendesha kipindi hicho. Baada stori na kuchagua nyimbo mbili tatu ikafikia wakati akaamua kumwambia VJ kwamba ampigie wimbo wowote wa Immortal Technique. Kilichotokea ni kwamba yule VJ hakucheza wimbo wa Immortal bali aliucheza wimbo wa Jay Moe aliomshirikisha Mangwea uitwao "kimya kimya".
Nilichojifunza ni kwamba kwenye hili game la Tanzania Jay Moe ni msanii pmaarufu kuliko Immortal Technique. Pia Madj wengi wa sasa ni "waweka kanda" kama Vital Maembe anawaita na sio wafuatiliaje wa muziki na ndio maana Vj akashindwa kutofautisha kati ya Immortal Technique na Jay Moe nadhani alidhani Kala Pina kasema Moe Technique ambayo pia ni "a.k.a" ya Jay Moe.
Enewei, Juma Mchopanga au maarufu kwa jina la Jay Moe ni mchanaji ambaye analijua hili game tangu hajaanza kulicheza. Inaaminika ameanza kulicheza mwaka 1998 ikiwa ni miaka ishirini tangu azaliwe mnamo tarehe 27/11/1978. Muziki huu ambao umeanza kushika kasi mwanzoni mwa miaka ya 90 kuna uwezekano mkubwa Jay Moe akiwa na miaka kumi na kitu akawa analifuatilia game kwa ukaribu kwahiyo yupo sawa anaposema analijua kabla hajaanza licheza.
Kuna taarifa zinaeleza kuwa, Mwaka 1999 alianzisha kundi lililoitwa Underground Kingdom na baadaye wakalibadilisha jina likaitwa Sewer Celibracy akiwa na Jaffarai na Mchizi Mox. Mwaka 2000, Jay moe na kundi lake walishiriki katika mashindano ya kutafuta vipaji yaliyoandaliwa na Clouds Fm huko ndiko walikokutana na Mack 2 B, Lady Lou na Solo Thang wakaunda kundi la Wateule baada ya kushinda na kupata nafasi ya kurekodi album chini ya Bongo Records.
Jay moe tangu ameanza gemu mwaka 98 mpaka leo yupo katika gemu huku kukiwa hakuna dalili zozote za kusanda. Naamini hili hata yeye alilijua mapema ndio maana akaamua kujibatiza jina la Mbakiaji. Mashabiki ni mashahidi wazuri kwamba wengi wasanii wamekuja wamemuacha na bado ngoma zake hazijachuja bado zinabamba japo zina miaka kibao.
Jay moe yupo kwenye hili game kabla Mamu hajaanza kugonga nakala za album. Mamu au kwa jina maarufu kama mdosi chini ya kampuni yake iitwayo GMC wasanii promoters Ltd iliyosajiliwa miaka tarehe 03/01/2001 (miaka mitatu baada ya Jay moe kuanza game) na kupewa 40577 ni moja kati ya kampuni za kwanza kwanza kuanza kusambaza kazi za wasanii wa Tanzania.
Album ya kwanza ya Jay Moe iitwayo “Ulimwengu ndiyo mama” iliyotoka mwaka 2002 ilisambazwa na GMC ikiwa na vibao kama “Ulimwengu ndiyo mama”, “Mi Mshamba”, “Maisha ya Boarding ft Dully sykes”, “Bishoo”, “Kama unataka demu”, “Misosi, mitungi na pamba ft Ay”, “Mpenzi kwaheri”, “Safari njema”, “Ulimwengu ndio mama rmx” na “Mvua na jua”.
“Mawazo ya Jay Moe” ni albamu yake ya pili iliyotoka mwaka 2005 na kusambazwa pia na wadosi pia (GMC) huku album yake ya tatu “Mocumentary” haikuwahi kutoka japo ilitangazwa tangu mwaka 2007. Jay moe aliwahi kusema kwamba ameshindwa kutoa album yake ya mocumentary kama alivyoahidi kutokana na kukosekana kwa mwamko kwa wasanii kutoa album badala yake wamekuwa wakitoa singo kwa sababu ya mabadiliko ya biashara ya muziki (Ayo, 2015)
Inawezekana pia album yake haikutoka kutokana na msambazaji ambaye alimsambazia album yake ya kwanza na ya pili kuachana na usambazaji wa nyimbo za muziki wa kizazi kipya. Ruge (2013) aliwahi kusema “Gmc.. sasa hivi ni mwaka wao wa pili na nusu hawajatoa hata album moja ya bongo flava wanafikiri kwa mamu pamefungwa lakini mamu anaendelea na wasanii wa Gospel na wanauza vile vile”.
Wakati Jay moe anatoa album ya kwanza “Ulimwengu ndio mama” mwaka 2002 chini ya GMC msanii mwenye album alikuwa anapokea Tsh 100 kwa kila tape ambayo ilikuwa ikiuzwa 1,200. Pia katika album ya pili “Mawazo ya Jay Moe” ya mwaka 2015 msanii mwenye album alikuwa akilipwa Tsh 200 kwa kila kanda iliyokuwa ikiuzwa Shilingi 1500 (Dudubaya, 2010)
Itaendelea............
Imeandikwa na
Malle Hanzi
O715076444
©2016
Powered by @babalaoTV www.babalaoinc.blogspot.com