Saturday, April 29, 2017

Alichokisema Fid Q kuhusu Sakata la Bongo Movie na Movie za Kigeni (WWW.BABALAOINK.BLOGSPOT.COM)

Moja kati ya habari kubwa sana ambazo zinatrend kwasasa Bongo Tanzania ni pamoja na sakata la kuzuiwa kwa movie za nje ambazo zinatafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambazo zinadaiwa kuharibu soko la filamu za ndani.
Mengi tumeyasikia na wengi wameongea, ila mkali wa Hiphop Tanzania Fareed Kubanda almaaruf kama Fid Q naye alikuwa na yakwake ya kusema kupitia kipindi cha leo Tena cha Clouds FM hapo jana.
Fid Q amepongeza harakati ambazo zinafanywa na mastaa wa Bongo Movie na kudai kwamba wanahitaji kusapotiwa juu ya hilo na pia akawapa ushauri mdogo ambao yeye anahisi unaweza kuwa msaada kwao.
Kimoja kati ya vingi ambavyo Fid Q amewashauri Bongo Movie, ni kujipanga na kuwa kama team moja na kutoa kazi zao kwa mpangilio ili kuzi-push kazi hizo na kuhakikisha zinafika mbali tofauti na kuwa kwa wiki wanatoa filamu 5 au 10.

No comments:

Post a Comment