Saturday, April 29, 2017

Jux akanusha tetesi za Kuachana na Vanessa Mdee(WWW.BABALAOINK.BLOGSPOT.COM)

SIku chache zilizopita zilizuka tetesi kwamba mastaa wawili wa muziki ambao wako katika mahusiano ya kimapenzi, Vanessa Mdee na Jux wameachana.
Tetesi ambazo zilizua gumzo katika mitandao ya kijamii, ikiwa hatukupata kauli yoyote kutoka kwa wahusika hao wawili.
Kwenye XXL ya Clouds FM Jux alikuwepo kutambulisha ngoma yake mpya ambayo ameipa jina la Umenikamata, na moja kati ya maswali ambayo aliulizwa ni kuhusu tetesi za kuvunjika kwa mahusiano yake na Vanessa.
Jux amekanusha tetesi hizo na kudai kwamba wao wako vizuri, ila tu ni tetesi ambazo zimezuka baada ya kutoonekana kuwa karibu na Vanessa kwa muda sasa.

No comments:

Post a Comment