Thursday, March 2, 2017

Jipange kumuona Vanessa Mdee kwenye Season 5 ya MTV Shuga ‘Down South’ mwezi huu

Lile shavu alilopata mwanadada Vanessa Mdee mwishoni mwa mwaka jana la kuigiza kwenye tamthilia ya MTV Shuga Afrika Kusini kwenye msimu wa tano, hatimae njiani kutoka. Vanessa Mdee ni miongoni mwa sura mpya za kuzitegemea kwenye series hiyo.
Kama ulidhani kuwa kipaji pekee cha Vanessa Mdee ni kuimba basi jiandae kwa ma-surprise kwani msimu wa tano wa series ya MTV Shuga ‘Down South’ itakuacha mdomo wazi ukijiuliza maswali mengi sana juu ya uwezo wake wa kuigiza.
Kwa mujibu wa series hiyo, Vanessa atauvaa uhusika wa mwanadada aitwaye ‘Storm’, na hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Watanzania kumuona Vanessa Mdee akiigiza pia itatusanua uwezo wake mwingine tofauti na uimbaji.

Storm ni nani?

“Storm ni kipenzi cha kila mtu, mrembo mwenye mvuto wa kumpagawisha mtu yoyote akatizae mbele yake. Mbali na uzuri wake Storm ameolewa na Rakeem, lakini maisha ya ndoa yanaonekana kutokompendeza sana mrembo huyo kutoka Tanzania. Uwezo wa Rakeem kushindwa kuonyesha mapenzi ya kutosha yanamuacha Storm akitafuta mapenzi hayo sehemu nyingine. Ujio wa Femi unakuja kwa wakati sahihi kwa Storm. Je, Storm na Rakeem wataweza kuiokoa ndoa yao? Au ujio wa Femi utavuruga kila kitu.”
Vanessa ataungana na wasanii wengine kwenye tamthilia hiyo akiwemo Thuso Mbedu, Mohau Mokoatle Cele, Jezriel Skei, Emmanuel Ifeanyi, Nicki Mutuma na Adesua Etomi.
MTV Shuga ‘Down South’ itaanza kuonekana kuanzia tarehe 08 March 2017 exclusively kupitia chanel ya MTV Base (DSTV Channel 322) na BET (DSTV Channel 129).

No comments:

Post a Comment