Thursday, March 2, 2017

WIZKID AUNGANA NA ALI KIBA.

Starboy mwenye star love duniani kutoka pande za Naijaa Wizkid amedondoka mkataba mnono na Kampuni ya Sony International.
kupitia mtandao wa RocStar4000 umethibitisha Star boy  anayetesa na jiwe la Sweet Love kusaini kandarasi ya  kufanya kazi na kampuni hiyo kubwa ya Entertainment duniani.
Hii itakuwa ni habari kubwa kwa mtoto wa Kkoo  Ali kiba sasa anaweza kupata nafasi wakafanya kollabo matata na mkali huyo wa kutumbuiza duniani.
Alikiba mwenye tittle best Aftican Act MTV Ema na Wizkid mwenye tittle ya Best Worldwide Act kupitia MTV EMA huenda ndiyo Mwanzo wa Kuzima Kelele za mashabiki wao ambao walitofautiana mwanzoni baada ya MTV EMA kumpatia kimakosa Tuzo aliyoshinda Alikiba kupewa Wizkid.
Mashabiki wanasubiria kolabo tu washikaji si wapo chini ya  lebo moja ni mipango tu kwa menejimenti Kama itaamua kutengeneza kolabo la wakali hao.

No comments:

Post a Comment