Saturday, October 29, 2016

Alikiba na ujio mpya wa Abby Skillz (WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Abby Skillz ni msanii mkongwe wa Bongo Fleva ambaye aliwahi kupata nafasi ya kuhit na ngoma zake kadhaa kipindi cha nyuma.
Kimya cha muda mrefu ndio jini ambalo lilimkumba Abby Skillz na kujikuta akipoteza kabisa nafasi yake katika game ya music kutokana na muziki kubadilika na wasanii wakali kuongezeka kila iitwayo siku.
Kutokana na makubwa ambayo aliwahi kuyafanya Abby Skillz wakongwe wenzake Mr Blue pamoja na Alikiba hawakusita kumshika mkono na kumpa msaada ili kuhakikisha mkali huyo anarudi katika ramani ya music na anasimama imara kama ilivyokuwa zamani kutokana na kuamini kwenye uwezo wake. Ndipo walipoamua kukaa chini na kutengeneza ngoma ambayo wameipa jina la Averina.
Jana wakali hao watatu walikuwa katika media tour kituo cha Clouds Fm katika kipindi cha Leo Tena, ndipo Alikiba alizungumza haya kuhusu ujio mpya wa mkali huyo.
“Muziki umechange lakini kuna wasanii wakongwe ambao hawajui kama muziki umebadilika, wasanii wakongwe kama kina Abby Skillz wapo wengi, na wengi wameshajaribu kurudi tena lakini wanashindwa kufika zile levels ambazo watu wanazitaka sasa hivi, yote ni kwasababu hawajagundua ni kitu gani ambacho sasa hivi kinaendelea. Wanachotakiwa ni kusoma alama za nyakati kisha wasanii ambao wapo katika game wasiache kutoa sapoti kama mimi na Mr Blue tulivyotoa sapoti kwa Abby Skillz.”
Hayo ni machache tu kati ya mengi ambayo yamezungumzwa na Alikiba.

No comments:

Post a Comment