Thursday, June 8, 2017

MSANII KUTOKA AFRIKA AKABIDHIWA JUKWAA KUELEKEA TUZO ZA BET [WWW.BABALAOINK.BLOGSPOT.COM]

BET wametoa orodha ya wasanii ambao watapanda katika steji ya utoaji tuzo usiku wa June 25 Jumapili mwaka 2017.
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika katika jiji la (L.A)Los Angeles nchini Marekani katika ukumbi wa Microsoft Theater , Hata hivyo msanii tokea bara la Afrika Wizkid nae ametajwa katika watu watakao weza kushiriki kutoa burudani kwenye Tuzo hizo kubwa huku list hiyo ikiwa na wasanii nguli kama vile Snoop Dogg, Wiz Khalifa, Pusha T, Desiigner, Bryson Tiller, Rae Sremmurd, Jhené Aiko na New Edition.
Katika awamu ya kwanza BET wamewataja pia wasanii kama Migos, Bruno Mars, Future, Trey Songz na Tamar Braxton ndio watakaoanza kupanda kwenye stage kutoa burudani katika usiku huo.
Tamasha hilo litakalo fanyika siku nne mfululizo litaoneshwa mubashara kuanzia saa mbili usiku.Msanii Beyonce na Bruno Mars ndio walio ongoza kutajwa katika vipengele tofauti, Huku Beyone akiwania vipengele saba, na Bruno Mars akiwania vipengele vitano.
Pia wasanii kama Solange, Chance the Rapper na Migos,wakiwa katika vipengele vinne vinne.

No comments:

Post a Comment