Thursday, June 8, 2017

Juma Nature anafeli kwasababu anakosa kampani yangu-: Mkubwa Fella [WWW.BABALAOINK.BLOGSPOT.COM]

Kama wewe ni shabiki wa Bongo fleva kuanzia miaka ya 2000 na kuendelea naamini utakuwa unalikumbuka kundi la muziki la TMK Wanaume, kundi ambalo lilikuwa likivikutanisha vichwa kama Juma Nature, Chege, Temba na hata KR MUllah.
Kundi ambalo baadaye lilikuja kugawanyika na kuibua makundi mawili ambayo ni TMK Wanaume Family na TMK Wanaume Halisi ambapo Juma Kassim Kiroboto ndiye ambaye alikuwa kiongozi wa TMK Halisi ambao walionekana kama kujiengua hivi katika umoja ule wa mwanzo.
Ni ukweli usiofichika kwamba hakukuwa na mafanikio makubwa kihivyo katika safari ya Juma Nature na wenzie kutokana na wengi wao kuwa wamepotea kwenye game kulinganisha na wasanii kama Chege na Temba ambao walibaki katika uongozi wa kundi na hadi leo wanazidi kutusua.
Mkubwa Fella ambaye ndiye alikuwa meneja wa kundi la TMK Wanaume enzi hizo na kutaka kuujua mtazamo wake juu ya kushuka kwa msanii Juma Nature kimuziki ukilinganisha na nafasi aliyokuwa nayo kipindi kile.
“Yule muziki wake haujapungukiwa, yule kapungukiwa kampani yangu, sababu muziki wake ndio uleule aliokuwa anafanya na muziki ni uleule, ila kampani. Kwasababu mimi ninaweza kuongea na mwenye radio vizuri, mimi naweza kuongea na Dj vizuri, yeye anaweza akatunga mashairi vizuri. Kikubwa unaweza kutunga mashairi vizuri lakini ukawa hauna kauli nzuri ya kuongea na Dj ama Mtangazaji lakini mimi naweza kuwa nayo busara hiyo, lakini sio kwamba nyimbo zake ni mbaya.” ALisema Mkubwa Fella.

No comments:

Post a Comment