Thursday, March 2, 2017

VANESSA MDEE ANA ROHO MBAYA! EDU BOY.(WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM)

Underground kutoka Rock City Mwanza Edu boy ameyatoa ya moyoni katika ngoma yake mpya ya Naieee kuwa wasanii wakubwa wenye majina wanawazarau wasanii wadogo.
Akifanya utambulisho  wa ngoma yake mpya Edu boy amewafungikia wasanii mbalimbali na maproducer wanaobana nafasi kwa wasanii wadogo kuwanyimia mwanga wa kutoka.
Katika mahojiano yake hayo amesema hawezi kumsahau Vanessa Mdee alimuomba kumpostia cover ya ngoma yake lakini jibu alilopewa na Vanessa lilimkatisha tamaa ya kuendelea kufanya mziki.
Katika ngoma ya NAIEEE aliyomshirikisha Rapa kutoka LFLG, Bill Nass anasema kila kitu kilichopo kwenye ngoma hiyo ni maisha yake ya kweli kwenye maisha ya mziki.

No comments:

Post a Comment