Thursday, January 21, 2016

MOTRA ATAJWA NA DIAMOND KUA MSANII ANAETAMANI KUFANYA NAE KAZI [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Anaitwa GOODLUCK JOSEPH a.k.a MOTRA THE FUTURE ni msanii wa muziki wa HIP HOP kutoka jijini Arusha ila kwa sasa kazi zake za muziki anafanyia jijini Dar es salaam chini ya CLASSIC SOUND ya Producer Mona Gangstar.Jana majira ya mchana katika kipindi cha XXL ya CLOUDS FM,hitmaker wa ngoma ya JE UTANIPENDA hapa namzungumzia Chibu Dangote a.k.a Diamond alipoulizwa ni wasanii Tanzania anaotamani kwa sasa kufanya nao kazi,ndipo alipomtaja MOTRA kua miongoni mwa wasanii hao wakiwemo WEUSI kutoka Arusha na FID Q.
MOTRA kwa sasa jina limezidi kukua akiwa na management mpya tofauti na ile aliyokua nayo awali na sasa ana wimbo unaofanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio uitwao ONE DAY aliomshirikisha mwanadada RUBY.Kujua mengi zaid kutoka kwake usichoke kutembelea ukurasa huu wa kiburudani.
Powered by @babalaoTV www.babalaoinc.blogspot.com

No comments:

Post a Comment