Thursday, October 29, 2015

Tafakuri Ya Mwanatamaduni!! [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

NANUKUU..
Fid Q na Juhudi za Wasiojiweza.
KWANZA,Wote TUNAKUBALIANA kuwa hiphop/rap ni muziki wa harakati hasa kumkomboa mtu wa chini,,historia inaonesha hivyo,,hphp ni sauti ya wasio na sauti,hphp ni macho kwa vipofu ,hivyo basi hphp kwa miaka mingi imekuwa kimbilio la wanyonge na tabaka linalokandamizwa na utawala wa kibabe,,PILI wote TUNAKUBALIANA pia kuwa ccm ni chama ambacho kwa miaka yote kiliyopewa dhamana/kuiba dhamana? kimesababisha uduni na ugumu wa maisha kwa kiwango kisichoelezeka ktk nchii hii na kwamba sasa kinafaa kupumzishwa.LAKINI wote HATUKUBALIANI kwamba Chama cha democrasia na Maendeleo(Chadema)ndio kinafaa kukabidhiwa madaraka hayo,,wapo wanaoamini kwamba chama hiki kinafaa na wapo wanaoamini kwamba chama hiki(cdm) hakifai hata kupewa nafasi ya udiwani,,ndio maana sishangai kuona wapo waliompigia kura Hashim Rungwe.huo ndio ukweli wa mambo,,hphp haisemi kwamba Fid q kwa kuishabikia ccm basi anakuwa Wack Mc kama alivyokoment Chindo lkn pia haisemi kwa Chindo kushabikia ukawa au kumsema Fid wack basi yeye anakuwa konshaz, ,hphp haisemi kwa Fid kupiga picha na Rais Kikwete basi hafai kuwa mwana hphp akama alivyosemaga Nash,,na haisemi kwa Nash kutopiga picha na rais bas anafaa kuwa mwanahiphp,,hphp haisemi kwa Fid Q kumkebeh/kutokuwa upande wa Halima mdee basi hawezi kuwa Konshaz kama alivyonadi Malle lkn pia hphp haisemi kwa Malle kumkosoa fid au kumpigia debe Kingwendu/ukawa basi yeye ni konshaz,,na labda niende mbele zaidi,hphp haisemi ni sawa kwa wasanii wa hphp kuwapigia debe ukawa,,nini bongofleva maana hata msagasumu amefanya hivyo,,kinachoonekana ni juhudi tu za wasanii wachche wasiojiweza kujaribu kushawishi umma umkatae Fid Q kama mwanzo wasanii hawa walivyomponda Roma na leo wanamsifu viva roma,,msanii anapoishiwa hoja za kisiasa za kusema kwann mdee na sio warioba pale Kawe,,na kukimbilia kumshambulia mwenzake kwa kuhusisha na hphp huyo ni sawa tu na mtu anaetumia udini na ukabila ni mkinga tu
Nilisema hapo kabla,,kama wasanii hawawezi kuachana na mambo ya siasa kama walivyofanya weusi,,bas kila mtu awe huru kushabikia chama anachokitaka na kama wanashindana basi washindane kwa ilani,sera na itikadi za vyama hivyo na siyo kutumia kivuli cha hphp.mara huyu sio hphp,huyu sio konshaz huyu wack mc kisa tu hayupo upande wa chama chako,,huu ni ujinga wa kias cha chini kabisa.

No comments:

Post a Comment