Thursday, October 29, 2015

BARUA YA WAZI KWA FID Q. [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

NANUKUU KUTOKA KWA MALLE HANZI
Ni zaidi ya miaka kumi na tano sasa imepita tangu nilipoanza kukusikia na kukufuatilia; ingawa si muda sana umepita tangu tulipoanza kufahamiana na wewe.
nikukumbushe tu wewe ni msanii ambaye Mh. Profesa Jay (Mbunge wa Mikumi) alishawahi kusema ndiye umewainspire baadhi ya maemc mahiri wanaofahamika kwa sasa.
Kama umesahau naomba nikukumbushe pia wewe ni Mc ambaye ulishawahi kutajwa katika orodha ya maemc bora wa Hip Hop nchini Tanzania na wasanii wafuatao Jcb, Nikki Mbishi, One na Sterio kwa mujibu wa tovuti ya Tzhiphop.
Mbali na kutajwa kuwa mc bora wa hip hop na wasanii hao. Kuna watu wengi wengine wanakwenda mbali zaidi na kusema kuwa kimataifa wewe ndiyo unafahamika kama ICON WA HIP HOP YA BONGO.
Pia wewe ni msanii ambaye umekuwa ukinasibishwa na wewe ukijinasibisha mbele ya uma kuwa ni msomaji mzuri wa vitabu ndiyo tungo zake nyingi ni tata na zikijazwa mbinu nyingi za lugha na kupambwa na tamathali za semi. Hivyo amekuwa akipokea maswali mengi kutoka kwa wadau wa kiwanda muziki kuhusu tafsiri ya tungo zako
Usomaji wako wa vitabu na kunukuu maneno ndiyo uliosababisha mchanaji mmoja wa arusha ambaye alikuwa akitajwa kuwa na ushindani wa chini chini na wewe kukukebehi kuwa yeye hakopi mistari ya kwenye vitabu kama wewe.
Nikukumbushe kuwa wewe ndio uliyefikia hatua ya kusema wanaojiita makonshaz sasa hawajiiti hivyo tena kwa sasa wanajiita mangoshaz. Ukimaanisha ukonshaz sio ishu tena ishu ni ungoshaz, nisamehe kama nimekosea tafsiri.
Nimetafakari sana sifa zako hapo juu yaani KUINSPAYA, UKONSHAZI, USOMI WA VITABU, MC BORA WA HIP HOP TANZANIA, ICON WA HIP HOP BONGO, UFUNDI WA LUGHA nk.... nimeshindwa kuzilinganisha na hii post yako kuhusu Halima Mdee (mbunge mteule - Kawe)........
Itaendelea.....

No comments:

Post a Comment