Saturday, October 3, 2015

Je,nani atakuwa mrithi wa komba ccm,,na nani atakuwa komba wa upinzani?? [WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

ANAITWA IDDY MWANATAMADUNI NA KUPITIA UKURASA WAKE WA FACEBOOK KAANDIKA HAYA....NANUKUU

Tafakuri Ya Mwanatamaduni:
Nyimbo za Propaganda…….Tunapimaje Mafuta kwenye mzani wa Unga???
Nilipata kusema hapo kabla kuwa wasanii wanauhuru wa kujiunga na chama chochote kile na kukishabikia lkn ni bora kwao kama wangebaki kutoa elimu ya uraia na wawaache wananchi wajiamulie wenyewe kuliko wao kujipa uwakala wa vyama
Watu waliusifu wimbo wa Roma na kuziponda nyimbo za Inspector na chid,hiyo ni haki yao kabisa lkn bahati mbaya,hawakufanya hivyo kwa hoja za uzuri wa mashairi,bali kwa ushabiki wa vyama,,hapa ndipo tulipojikwaa,,inawezekana kweli vigezo vyetu vikabaki vilevile,,uandishi wenye kufata urari wa vina na labda mizani,ujumbe,midundo na mitambao? Hapana,,sio rahisi vile siasa imetawaliwa na ushabiki zaidi kuliko ukweli.sasa tunapima uzuri na ubaya wa nyimbo vigezo vya ccm na ukawa,wengine huenda mbali zaidi na kuwaponda wasanii binafsi,,eti Oh..Chid teja,na wanafanya hv wakiwa huku,lkn haohao wakiwa kule wanasema,,toeni hoja sio kuongelea afya ya mgombea??Miaka mingi tumekuwa tukilalama kwa redio kupima ubaya na uzuri wa nyimbo kwa mizani ya kurap na kuimba,,na sasa tunarudia kosa lilelile japo sio bongo fleva na hphp ila ccm na ukawa.kwa utamaduni huu wa kisiasa,mpinzani wako akitoa wimbo ni lazima uwe mbaya tu,kwa sababu yy ni mpinzani,hatuangalii midundo(mikito?)mitambao,uandishi,ujumbe,uwasilishaji nk.tunaangalia wimbo huu unasifu ccm au ukawa bhaaaas!!ubaya wa huu utamaduni ni kwamba;wasanii wanakuwa na shabiki wapya(feki?) sio wa kufurahishwa na mashairi yao bali kwa kufurahishwa na uwepo wao ktk vyama vyao,,matokeo yake ni kwamba baada ya uchaguzi hakuna tena habari za siasa na shabiki wanakuacha mtupu
Nimalize kwa kujibu nilichoulizwa na Kali Mbaya,,
kwa mtazamo wangu nyimbo zote,ya Roma,inspector na Chid,mgosi na nyinginezo zipo sahihi,sababu nazipima ktk mizani ya kisiasa(sio-uchama),,mawe ya mizani ya kisiasa ni yale yale-propaganda-uongo-matusi-kashfa-kifupi siasa ni mchezo mchafu na nyimbo zote zinakidhi vigezo hivyo,kuna baadhi ya wasanii wamefikia had kutukanana wao kwa wao na wao kutukanwa,No way out,,ndio wamechagua mchezo huo na hizo ndio taratibu zake!!
Hapo kabla tulizoea kwaya za Kapten Komba ktk kushabikia ccm lkn ktk hphp akina Prof.J walikosoa kote bila kuwa na upande,waliangalia issue na sio mtu lkn sasa hv ni mamboleo,,sio tu bongofleva eti diamond na yamoto,nao wazee wa kufokafoka hawapo nyuma,Inspector na chid na upinzani hawapo nyuma hapa Msaga sumu mzee wa vigodoro,kule Roma na wale wenzangu na mimi “ngumu kumeza”,,,
swali la kujiuliza Je,nani atakuwa mrithi wa komba ccm,,na nani atakuwa komba wa upinzani??

No comments:

Post a Comment