Sunday, January 10, 2016

KIKAO CHA WASANII CHA KISANII.[WWW.BABALAOINC.BLOGSPOT.COM]

Muziki wa Bongo Fleva /hiphop ni muziki unaongelewa zaidi mtaani na hata kuchezwa zaidi katika media house za ndani na nje ya nchi pia.Ila wapo walio wengi wasiojua mziki huu ulianza lini. Bongo fleva/hiphop ulianza miaka ya 1990 hasa ikiwa ni muigo wa kutoka kwenye muziki wa Marekani.DJ Show ndio kilikuwa kipindi cha kwanza kucheza nyimbo hizi za bongofleva/hiphop kutoka hapa Tanzania ndani ya Radio One,Taji Liundi ndiye aliyekuwa mtangazaji wa kwanza kucheza muziki huu na hii ilikuwa ni miaka ya 1994.
Muziki huu umeendelea kukua siku baada ya siku na sasa umegeuka kuwa biashara kubwa, na hata kuona wasanii wengi wakiwa wananufaika na huu muziki tu.Licha ya mafanikio wanayopata lakini bado wana haki nyingi ambazo wanapoteza ambapo kama Serikali ingesimamia swala hili basi leo tungekuwa na wasanii milionea kupitia mziki huu wa kizazi kipya.
Wapenda utani husema eti kila nyumba ina msanii mmoja wa muziki wa kizazi kipya,huwa nacheka mwenyewe tu kila nisikiapo mtu akisema hivyo.Ukifuatilia kwa makini ni kweli kuna wasanii wengi sasa katika kila upande na yote hii ni baada ya kuona pia muziki umekua ajira.
Vinega ambao walifanya mixtape ya Ant Virus walikuwa watu wa kwanza kuzungumzia kuhusu wasanii kulipwa mirabaha.Nadhani hawakupata support kubwa kutoka kwa wasanii wengine kutokana na matumiz ya lugha kali katika tungo zao nyingi ambazo
zilielezea unyonyaji uliopo katika muziki wa bongo fleva ,Hiyo ilikuwa ni miaka ya 2010 na kuendelea.
Pia miaka hiyo kulikuwa na fursa nyingi hasa wasanii walipata nafasi ya kuulizwa na Rais mstaafu Mh Kikwete matatizo wanayokutana nayo kila siku na majibu makubwa yalikuwa studio.Kitu ambacho hakileti maana hivi kweli studio ni tatizo kwenye mziki?na studio ikatolewa, Je mpaka sasa mnajua studio iko wapi?na ni msanii gani unajua amewahi kufanya kazi katika studio hiyo?.Hii ni kwa mujibu wa Mr II Sugu pamoja na Mgosi Mkoloni.
Pia Mgosi Mkoloni aliwahi kusema” kwenu yinyi mashabiki mnatakiwa mjue mziki una nini ndani yake,Game ilianza vizuri sana na wengine hata hawakuwepo ila walivutwa na game kutokana na waliokuwepo lakini leo wamebadili upepo,hatuendi kihivyo mwanangu kaa ukijua mziki unalipa tena sana mbali na kufanya mziki tunahitaji hela, na huwezi kutumia kipaji cha mtu kujinufaisha wewe mwenyewe hilo ni kosa la jinai”. Turudi kwenye lengo haya mengine ni mambo tu niliyotaka watu makini tujiulize.
Sababu nyingine ambayo ilifanya zoezi la kulipwa mirabaha kukawia ni kukosekana kwa mitambo ya kujua wimbo/nyimbo zimechezwa mara ngapi katika kituo cha radio au tv husika.Wapo waliolaumu Cosota kuhusu hili jambo,lakini ukweli hujitenga na uongo pale ambapo mkurugenzi wa Cosota aliposema “hatuna mitambo ya kufuatilia radio na tv zimecheza mara ngapi wimbo sasa hapo tunawazaje kukusanya mirabaha?”
P Funk Majani mtayarishaji mkongwe katika muziki wa kizazi kipya,ambaye ndiye mtayarishaji bora wakati wote na amekuwa na kumbukumbu za pekee katika muziki huu.Pia ni mtayarishaji anaeongoza kuandaa album nyingi katika muziki huu kizazi kipya. Mwaka 2014 -2015 P funk Majani walitambulisha CMEA ambayo walieleza mipango mingi mizuri na hata mwaka jana kuanza kufanya kazi kwa kushirikiana na Cosota.Hii ni katika kutekeleza swala la wasanii kulipwa mirabaha
CMEA kazi yao kubwa ilikuwa ni kujua kuwa wimbo wa msanii Fulani umechezwa mara ngapi kwa siku wiki na hata mwezi,na P funk alieleza mitambo hiyo inanasa na kutunza kumbukumbu ya muda wa wimbo wa msanii ulipochezwa.Hapa kila mmoja alipata kuona sasa neema imefika kwao wasanii.
Tarehe 12/12/2015 kulifanyika semina ilichojumuisha Cosota,CMEA pamoja na wasanii wa bongofleva/hiphop.taarabu,bendi,kwaya,na mkutano huo uliudhuliwa na wasanii wengi wa kizazi kipya.
Mwana Fa ni moja kati ya wasanii walipata nafasi ya kuongea katika semina hiyo ambapo alisema “ebwana aah si wengine tumefanya muziki wa muda mrefu kidogo na hivi vitu mwazoni vilikuwa vinaonekana kama ndoto,kwaiyo hatua ilipofika tuwapongeze CMEA na Cosota.”
Wengine ambao walipata nafasi ya kuongea ni pamoja na Lamar,Babu Tale, Nikki wa pili,Chaba,Jay MO,na wengine wengi
Hakika wote hawa walisifia kile kilichokuwa kinafanywa na CMEA.Hata kufikiria mapema mwaka huu kutakuwa na malipo ya mirabaha bila shaka.Nini kimewakuta wiki hii kusema hawana imani tena?Kwa maana hata Mh Nape aliwathibitishia wasanii kuanza kulipwa mirabaha mapema mwaka huu.Na pia wasanii walionekana kufurahishwa na maneno hayo na wengi kupost katika mitandao ya kijamii kuonyesha furaha yao.
Mwaka 2016 umeanza kinyume na matarajio yalikuwa ni ya watu wengi wapenda muziki pamoja na wasanii wenyewe.
Ni wiki kadhaa tangu ifunguliwe account katika mtandao wa picha instagram iliyoitwa wasaniitz ambayo kwa mara ya kwanza page hiyo ilitambulishwa msanii Nikki wa pili,ambayo kwasasa amefuta post hiyo ya utambulisho na hatuji kwanini amefuta sina kumbukumbu nzuri kwa alichokuwa ameandika lakini nadhani alisema follow page ya wasanii tz
Mpaka sasa ninapoandika makala hii ya wasanii na kikao cha kisanii page hii inafollowers 1739 wakati ikiwa imefollow 262.Na pia wiki chache baadae walipost tangazo kwenye page na kuandika”Kesho kuna semina THT kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa nane mchana juu ya biashara ya muziki na kuhusu na mirabaha,unaombwa kuudhuria na muhimu sana kwa manufaa ya muziki na wasanii.”
Hapo vipi ushaanza kupata picha ya wasanii na kikao cha kisanii?.Hivi kweli unaweza kuitisha kikao katika page iliyofunguliwa ndani ya siku kadhaa ambayo hata haijulikani?ila hapa watasema et ooh tulisema kupitia page ya wasaniitz,hii ni zaidi ya kichekesho.Na baadae walizanza kupost picha katika page hiyo wakisema “semina ya wasanii @chegechigunda lakini katika picha hiyo ilimuonyesha Mwasiti,Ditto na mtu mwingine ambaye sijaweza kumtambua lakini alifuatiwa na Madee.
Post ya mwisho ilimuonyesha Barnaba na kusema “barnaba akichangia kwenye semina” Mpaka semina inaisha nikaendelea kutazama page hiyo ya wasaniitz na mpaka wanamaliza hakuna ambacho walisema zaidi ya zile picha tu na maelezo mafupi.
Bado hujapata tu picha ya wasanii na kikao cha kisanii? Haya tuendelee tu utaelewa
Wiki moja baadae hii ni baada ya semina iliyofanya pale THT wakaweka tangazo kuhusu kikao kilichofanyika jana mataa ya St Peter Osterbay na kutaka wasanii wafike kwa wingi na tangazo hili lilipostiwa pia na wasanii waliowengi pamoja na baadhi ya wadau kadhaa.
Kwa bahati mbaya me sio msanii na wao walitaka wasanii tu kwahiyo sikuweza kuudhuria katika kikao hicho cha wasanii cha kisanii.Lakini yaliyoendelea nilipata kuyajua ambapo walifikia maadhimio matatu 1 ni kutokuwa na imani na CMEA 2.Kuvunjwa kwa bodi ya Cosota 3.Radio stations kuendelea kupiga nyimbo zao bure mpaka watakapotoa tamko.
Hapa ndipo tunapota wasiwasi juu ya kikao cha wasanii,Ambacho ni wazi kinaonyesha ni kikao cha kisanii yani kikao flani cha kuzuga tu lakini nyuma ya pazia watu wana manufaa binafsi sio kwa kila msanii.Kwanza kama kikao cha kwanza kilijumuisha wasanii wachache ambao ni wazi inaonekana walipanga agenda zao zenye manufaa yao, na baadae ndipo wakaitisha kingine ambacho taarifa zake zikaandikwa sana kuliko cha kwanza na hata katika uitishaji wake ulizungumziwa zaidi.
Kilichonishangaza zaidi katika kikao cha wasanii cha kisanii ni eti wasanii wamesema nyimbo zao ziendelee kupigwa bure,mpaka watakapotoa tamko.Hapa ndipo unapoona ndani yao kuna tatizo ambalo haliwezi kuisha leo wala kesho.
Cmea na wasanii kwangu naona ni kama mwaka flani ilitokea flevaUnit na Tuma.Tuma ni chama cha muziki wa kizazi kipya ambacho mpaka sasa sijapata kujua msemaji wa chama hicho ni nani maana imekuwa ni jambo la kawaida msanii Nikki wa pili kujivisha majukumu yasiyo muhusu mara nyingi kujifanya msemaji.Nadhani ni Nikki ni msemaji wa Weusi tu sio msemeji wa wasanii wote au Tuma.
CMEA imefanya kazi kwa muda mfupi sana na ikaonyesha umahiri pale inapojua kazi ya msanii Fulani imechezwa mara ngapi katika kituo chochote cha radio.Kitu ambacho wasanii au jamii haikuwa inajua ni mara ngapi wimbo umechezwa kabla ya Cmea kuanza kazi.Sasa unasemaje huna imanI na CMEA ?wakati bado unaendelea kupost takwimu zao kuhusu nyimbo yako kuchezwa katika media house?unapoendelea kutumia inamana unaamini kile wanachofanya.Hii ndo ile tunasema akili inataka lakini mwili hautaki.
Kinachofanyika hapa ni mahesabu madogo tu,watu wanacheza na akili za wasanii.Mtu mwenye manufaa amekaa pembeni anacheki mchezo tu jinsi wanavyojikanyaga wakati yeye akila keki vipande vyote.
Kikao cha wasanii nilitarajia kuona wasanii wakiongeza mikakati zaidi katika kulipwa mirabaha au kuongeza mawazo katika Cmea na Cosota, sio kufikia maamuzi hayo ambayo ni wazi ni maamuzi ya mtu aliyenje kisanii yani mdau kutumia baadhi ya wasanii kukwamisha hilo zoezi.
Au imeonekana CMEA ni mnyonyaji swali dogo tu jamani.Hivi kweli mnyonyaji wa wasanii hajulikani?au ndo wasanii kukosa msimamo na nafsi zao kutawaliwa na uogo mpaka wanashindwa kuwa na misimamo?
Kwa maadhimio haya lazima niseme kikao cha wasanii cha kisanii.Pia baada ya wiki mbili wamesema watachagua baadhi ya viongoziau wawakilisi wao katika kikao hicho cha wasanii.Hapa ndipo kichekesho kingine utakiona pale ambapo meneja wa msanii anapopewa ameneji mziki mzima hahahaha tucheke kabisa,na pia utaona Yule msanii anayetaka kuonekana anajua zaidi wakati aliwahi kufanya project ndogo tu ya fichuka ikamshinda leo ataweza hili?tukiongea tujifunze kubakisha maneno.
Lengo ni kujenga sio kutengeneza mfumo wenye kunufaisha wachache kila iitwapo leo.Wasanii na kikao cha wasanii.leo tuishie hapa tutaendelea.
Imeandikwa na
BATRO MBULINYINGI.
JANUARY 7, 2016

No comments:

Post a Comment