Thursday, April 24, 2014

BARUA YA WAZI KWA MA MC WOTE WA HIP HOP KUHUSU BUNGE LA KATIBA ISOME HAPA

BARUA HII IMEANDIKWA NA MMOJA WA MA MC KUTOKA ARUSHA 
***BARUA YA WAZI KWA MA-MC WOTE KUHUSU BUNGE LA KATIBA***
-kwenu ma-mc wote wa hiphop
kuna mawazo mengi sana ambayo mnayaibua kuhusu bunge la katiba na kims...ingi hayana mantiki...kwa mfano wengi wenu mnasema kwamba hamuangalii na wengne mnashawishi watu kufanya kama mnavyosema
swali la kujiuliza hapo ni
1; je, pasipo kujua yanayoongelewa kule ndani na kuyaelewa mtawezaje kukosoa au kurekebisha pindi rasimu hiyo ikiletwa kwetu wananchi?
2;je,rasimu inayojadiliwa kule inamhusu nani? Kama sio sisi
baada ya hapo ni lazima mkumbuke kuwa...KULIKIMBIA TATIZO SIO NJIA YA KUTATUA..ni lazima mkubali kwamba katiba bora ya tanzania itategemea mawazo ya mtanzania mwenyewe!
AMKENI MA-EMC WOTE MNAOJIITA WANA-HIP HOP..tambuen mnayoongea kla siku kwenye mitandao ya jamii yana "influence" kubwa kwa jamii...msijitie majinuni kwa ujinga wa "likes" mnazopata kwa washkaji zenu wasiojua maana ya mikumbo wanayofwata..
"KUWA NA BUSARA NI KUWA NA UJASIRI WA KUSEMA UNACHOJISKIA BILA WOGA" lakini kuwa na BUSARA NA HEKIMA NI KUCHAGUA NA KUFKIRIA UNACHOTAKA KUFANYA....
natumain mtaelewa na mtarekebika... Kwa wale wazimaji sio mbaya mkizima na hii!
Willey nazzareno...

No comments:

Post a Comment